• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

MSIMAMIZI WA UCHAGUZI SONGEA DC AWASISITIZA WANANCHI KUDUMISHA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

Tarehe ya Kuwekwa: November 14th, 2024


Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya wilaya ya Songea , Bi Elizabeth Gumbo, amefanya mkutano na waandishi wa habari leo akisisitiza umuhimu wa kudumisha amani na utulivu kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba mwaka huu.

Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri, ambapo Bi Gumbo ameeleza kuwa jumla ya vyama tisa (9) vimejitokeza kuchukua na kurejesha fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Vyama hivyo ni CCM, CHADEMA, CUF, TADEA, ACT Wazalendo, UDP, Demokrasia Makini, NCCR Mageuzi, na TLP.

Kwa mujibu wa Gumbo, Halmashauri ya Wilaya ya Songea inajumuisha jumla ya vijiji 56, na wagombea 97 wamejitokeza kugombea nafasi za uongozi kutoka vyama hivyo mbalimbali. Aidha, jumla ya vitongoji 443 vimeorodheshwa na wagombea 556 wameshajaza na kurejesha fomu kwa ajili ya kugombea nafasi katika vitongoji hivyo.

 Gumbo amebainisha kuwa zoezi la uteuzi na usikilizwaji wa rufaa linaendelea mpaka tarehe 15/11/2024 ambapo kampeni zinatarajiwa kuanza rasmi tarehe 20 hadi 26 Novemba mwaka huu.

"Vyama vya siasa vimeshaagizwa kuandaa ratiba inayoonesha ni wakati gani chama fulani kitakuwa mahali fulani kwa ajili ya kufanya kampeni. Tunawaomba vyama vyote tisa kufanya kampeni za kistaarabu kwani lengo letu ni kupata viongozi bora, na hatutarajii kuwa na changamoto au migogoro baina ya vyama wakati wa kampeni,” alisema Bi Elizabeth Gumbo.

Katika hotuba yake, Bi Gumbo pia ametoa wito kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea ambao wamejiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi ifikapo tarehe 27 Novemba 2024s, kuanzia saa mbili kamili asubuhi, ili kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka. Ameongeza kuwa Halmashauri imejipanga kuhakikisha '4R' za Mheshimiwa Rais zinafanyiwa kazi kikamilifu kwa faida ya wananchi.

Kwa ujumla, Bi Elizabeth Gumbo amesisitiza umuhimu wa amani, utulivu, na ushirikiano wa vyama na wananchi wote katika kuhakikisha uchaguzi huu unakuwa wa amani na wenye mafanikio.

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • MKIMBIZA MBIO ZA MWENGE KITAIFA, AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    May 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SONGEA DC, LIMEMSHUKURU MHE. RAIS NA WAZIRI WA AFYA KWA KUIHESHIMISHA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    April 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KULA YAMEANZA SONGEA DC

    April 29, 2025
  • MHE . JENISTA MHAGAMA AZINDUA MADARASA 27 NA VYOO MATUNDU 44, SONGEA DC

    March 16, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa