Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu( Sera Bunge na Uratibu) , ambaye pia ndiye Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Mhagama, amezindua Mradi wa kuendeleza Lishe na Ufugaji endelevu wa viumbe maji kwa Wakulima wadogo Songea.
Mradi huo ulioko Halmashauri ya Wilaya ya Songea, katika Kata ya Mpitimbi Ulihidhuliwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexanda Mnyeti, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe Ahmed Abbas Ahmed, Mwenyekiti wa CCM Mkoa , Mhe. Oddo Mwisho na Viongozi wengine wa Serikali
Timu ya Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mhe. Menans Komba, pia Mkurugenzi Mtendaji walikuwepo kazitaka uzinduzi wa Mradi huo, ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Songea kata ya Mpitimbi ndipo ulipo Mradi huo wa Ufugaji endelevu wa Viumbe maji.
“Leo tunazindua Shamba darasa ambalo litaenda kuchagiza maendeleo ya tabia nzuri ya biashara na matumizi ya lishe bora kupitia samaki wanaofugwa kwenye mabwawa na miradi itakayofanyika katika halmashauri yetu ya Wilaya ya Songea na Halmashauri nyingine kwa kadri tutakavyoomba
“Serikali imetoa kipaumbele kwenye Sekta ya Kilimo nchini, kupitia mradi wa awamu ya awamu ya pili ya program kuu ya kuendeleza Kilimo, na kama nilivyosema mwanzo Mradi huu ni sehemu ya Miradi hiyo mikubwa tumeamua kutenga Rasilimali fedha. Kama mnavyomuona Rais wetu, anahangaika kukuza mahusiano ya Kidemokrasia katika R zake nne na mabadiliko chanya ya maisha ya watu kwa ujumla wake “
Aidha Mhe Jenista alitoa wito kwa vijana na kina Mama wote wa Mkoa wa Ruvuma hasa Halmashauri ya Songea, kujitokeza kujifunza mradi wa samaki kupitia shamba darasa hilo.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa