Mpango wa BAJETI wa Juni 2020 /2021
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma limepitisha zaidi ya Sh.bilioni 23 za mpango na bajeti ya maendeleo ya mwaka wa fedha wa 2020/2021.
Mpango huo umewasilishwa na Kaimu Afisa mipango Charles Mihayo katika mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Bw Mihayo ametaja vyanzo vya mapato hayo kuwa ni makusanyo ya mapato ya ndani,Ruzuku toka Serikali kuu,pamoja na Ruzuku ya fdha za miradi ya maendeleo.
Amesema bajeti imelenga katika kutekeleza majukumu mballimbali kipaumbele ikiwa ni kukamilisha miradi viporo ikiwemo kukamilisha Ujenzi wa Zahanati 7,Vituo vya Afya 4 na ujenzi wa Hospitli ya Wilaya,kuajiri wa watumishi 788 katika kada mbali mbali,kuboresha na kuendeleza Usafi wa mazingira.
Maeneo mengine ni ujenzi wa miundombinu ya Elimu ya Msingi na Sekondari na mapambano dhidi ya Utapiamlo.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Rajabu Mtiula ametowa wito kwa wataalam kuhakikisha wanasimamia vema ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kudhibiti mianya mibovu ya ukusanyaji mapato endapo itajitokeza
Imeandaliwa na JACQUELEN CLAVERY
K / AFISA HABARI SONGEA DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa