Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe Wilman Kapenjama Ndile amekabidhi vishikwambi kwa Wahesh. Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya songea katika Mkutano wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024 wa Baraza la Madiwani uliofanyika tarehe 31/10/2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya songea.
Akikabidhi vishikwambi hivyo Mkuu wa Wilaya ya Songea ameiomba kamati iweze kuwafikiria Madiwani hao kuwaachia watumie tu vishikwambi hivyo hatakama muda wao wa kukaa madarakani utakuwa umekwisha kwani wanafanya kazi ngumu sana ya kuwahudumia wananchi hivyo hiyo kwao iwe kama motisha ya utendaji kazi wao. Amesema
“Labda niwaambie tu ukweli ndugu wajumbe hakuna viongozi ambao wanafanya kazi katika mazingira magumu kama Madiwani sio kama mwajiriwa ambaye anakuwa na uhakika wa kazi yake kwa muda mrefu hivyo mimi niwaombe kamati iliyoamua kuwapatia vitendea kazi hivi kurudi tena kwenye kamati yenu na kuona umuhimu wa watu hawa sio eti akimaliza madaraka yake basi akirudishe mi nadhani ni vyema wangeendelea kutumia ili iwe kama kumbukumbu na zawadi kwao ili waweze kufurahia matunda ya kazi zao wakati walipokuwa wakiwahudumia wananchi”.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndug Neema Maghembe alikubaliana na wazo hilo na kumuahidi Mkuu wa Wilaya atalipeleka kwenye kamati ili liweze kufanyiwa kazi.
Kisha Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya songea Mhe Simon Kapinga aliweza kuishukuru kamati kwa kuona umuhimu wa kuwapatia vitendea kazi Wahesh Madiwani ili viweze kuwarahisishia baadhi ya kazi pia amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Songea kwa kuwakabidhi vishikwambi hivyo. Amesema
“Kwaniaba ya Wahesh Madiwani nasema nashukuru na tunafuraha sana leo kwa kupokea vishikwambi kwaajili ya shughuli mbalimbali za halmashauri tunaamini sasa hututasikia kwamba kuna mtu atasema kwenye simu yangu haujaingia ujumbe wa taarifa ya kikao kwa kuwa tunaamini sasa kila taarifa itakuwa inaingizwa kwenye vishikwambi kwahiyo hili jambo ni jema na niseme limefanyika kwa wakati na muda sahihi”.
Baada ya zoezi hilo la ugawaji wa vishikwambi Afisa Tehama wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea John Luoga aliweza kutoa elimu juu ya matumizi ya kifaa hicho na jinsi ya kukituza ambapo aliwaomba watumiaji wa kifaa hicho watangulize uzalendo kwenye matumizi ya nyaraka za Serikali, pia amewaomba simu hizo zitumike kwaajili ya matumizi ya Kiserikali. Ambapo kila Mhe Diwani amekabidhiwa kishikwambi chake ambacho kina chaja yake na uwanja wa kuandikia (Key board).
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa