Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Kanali. Ahmed Abbas Ahmed, ametembelea na kukagua ujenzi Stand ya Kisasa iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Songea kata ya Peramiho.
Akisoma taarifa Mratibu wa TASAF, Wilaya Halmashauri ya Songea Bi. Hossana Ngunge alisema “Fedha kiasi cha shilingi Milion Mia nne thalathini na nne, laki sita hamsini na saba elfu mia nane na mbili na senti sitini na nane ( TSH. 434,657,802.68) ziliwekwa kwenye akount ya Halashauri kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu wa Stend ya Mabasi mnamo mwezi Juni mwaka 2022.
Fedha hizo ni kwa ajii ya ujenzi wa Jengo la Utawala, Maduka 36, Vibanda vya walinzi viwili, vyoo matundu nane (8) pamoja na uzio
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, baada ya kupokea taarifa, aliipongeza kamati ya ujenzi lakini pia msimamizi wa ujenzi wa Stend hiyo akisema.
" niwapongeze sana kwa usimamizi mzuri wa mradii huu, uliofanywa na viongozi lakini pia wanakamati nimekagua, nimepokea taarifa, tuseme nimefarijika sana kwa utekelezaji wa mradi huu, hasa ushirikishwaji wa wananchi toka hatua za mwanzo "
Lakini pia kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bi Hosana Ngunge alimshukuru Rais wa Jmamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. Samia Suluhu hassani kwa kuwaletea fedha za ujenzi wa miundombinu ya Stendi.
Shukrani pia zilitolewa kwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Mhagama kwa kujitoa kwake kwa ajili ya wananchi wake.
Pamoja na hayo Mratibu alimshkuru pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya WIlaya ya Songea, Mhe. Menans Komba, kwa ufuatiliaji wa miradi ndani ya Halmashauri ya Songea lakinin pia Diwani kata ya Peramiho kwa ushirikiano anaoutoa katika utekelezaji wa miradi ndani ya Kata ya Peramiho.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa