MKOA wa Ruvuma umezindua Jukwaa la wadau wa Usimamizi na uendelezaji wa Rasilimali za Maji katika Dakio la sehemu ya juu ya mto Ruvuma kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme.
Uzinduzi huo umefanywa na Katibu Tawala Msaidizi Jeremia Sendoro kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Chistina Mndeme uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha VETA Mjini Songea Mkoani Ruvuma.
Sendoro amesema ni fursa kwa wadau kujadili na kutoa maoni na mapendekezo ya namna ya kutunza vyanzo vya maji ili visiharibiwe.
Sendoro amesema kwa upande wa Serikali ya Mkoa wa Ruvuma imejipanga, wananchi wanaoishi sehemu ya mradi huu itahakikisha unatekelezwa,nakuunda jumuiya ya watumia maji, sheria za vijiji na Halmashauri ambazo zitalinda watumia maji wote ili asiwepo mtu wa kukosa maji au kupata maji kidogo kulingana na Mahitaji isipokuwa wote wafuate sheria zilizowekwa.
“Tutatoa maelekezo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri,watendaji wa Kata na Makatibu Tarafa na viongozi wote kuhakikisha wanatekeleza maazimio haya kwamba wananchi wa Ruvuma wanapata Maji na yasichafuliwe wala kupotea bila utaratibu, maji haya tumeyalithi kutoka vizazi vilivyopita nasi tuwalithishe vizazi vijavyo”.alisema Sendoro
Amesema usimamizi na utunzaji wa Rasilimali za Maji kwa mfumo wa mabonde unasimamiwa na Sheria ya Maji na11 ya mwaka 2009 kusimamia,kupanga,kuendeleza na kutunza Rasilimali za Maji nchi imegawanyika katika mabonde 9.
Mkurugenzi wa Bodi ya Maji ya Bonde la Ruvuma na Pwani ya kusini Sudi Mpemba amesema anao wajibu wa kusimamia rasilimali za Maji katika mabonde na utaratibu waliouanzisha wa kuzindua Majukwaa ya Mabonde na kusimamia Maji umeanza ngazi ya Taifa ni mwongozo wa sera ya mwaka 2002.
Amesema kutakuwa na mwongozo unaelekeza kusimamia Maji ngazi ya Taifa na na ngazi inayoifuata ni Madakio na ndiomana leo tumekutana na wadau kuzindua Jukwaa la usimamizi wa rasilimali za maji sehemu ya dakio la Mto Ruvuma kwa watumiaji wa sehemu ya juu ndiko kwenye chanzo cha maji sehemu ya matogoro na wanatumia Wilaya ya Mbinga,Songea,Nyasa na Namtumbo
Hata hivyo amesema kupitia jukwaa hili nikuwafanya wadau waweze kuzungumza namna bora ya kusimamia na kuendeleza rasilimali za maji bonde la Maji na kuangalia changamoto pamoja na kutatua Migogoro .
“Tunatambua watumia maji wapo wa aina mbalimbali kutoka kwenye mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali mfano shamba la kahawa Avivu,watumiaji wanaozalisha umeme,pia kuna wadau wa Halmashauri ya Mbinga, Nyasa na tupo hapa kuunda vikundi kwaajili ya usimamizi na tayari umeainisha kwenye mpango wa usimamizi na umekamilika na unahitaji kutekelezwa”.amesema mpemba
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya watumia Maji Bonde la Ndanda Andrew Mwanjela amesema Kwa Mkoa wa Mtwara wamejipanga lakini wanapata changamoto ya uelewa wa wananchi ni mdogo kwamba chanzo cha maji ni nini? na kutoa visingizio vya Elimu wakati wataalamu wanatoa kila mara,amesisitiza kupitia Jukwaa hili maamuzi yatolewe ili kulinda vyanzo vya maji na kuepuka uhaba wa Maji.
Imeandikwa
Jacquelen Clavery
Songea DC
Desemba 1,2020.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa