Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mwl. Neema Michael Maghembe, amekabidhi vitabu vya kiada kwa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi waliopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa lengo la Kuhimiza matumizi ya Mtaala ulioboreshwa, unaowahusu wanafunzi wa Elimu ya Awali, Darasa la kwanza na darasa la tatu.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea, imepokea vitabu vya Kiada vya Elimu ya Awali na Msingi Darasa la I, III na Mihtasari vya mtaala ulioboreshwa vyenye thamani ya shillingi 12,930,529/= kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania ( TET) ambapo Mkurugenzi Mtendaji amevisambaza kwa Shule zote za Msingi na kusisitiza matumizi ya vitabu hivyo na sio kuweka makabatini.
Akikabidhi vitabu hivyo kwa walimu hao katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji iliyopo Makao makuu ya Halmashauri Mwl, Maghembe alisema “Kwanza kabisa napenda Kumshukuru Mhe. Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa anazofanya kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora, Mhe. Rais amewekeza nguvu kubwa sana kwenye elimu, kwa kutujengea miundombinu iliyobora, lakini pia kutoa Elimu bure bila malipo kwa wanafunzi wote kuanzia darasa la awali hadi kidato cha sita
hivyo leo tumepatiwa vitabu vya mtaala ulioboreshwa baada ya mchakato mrefu kuusu martumizi yta mtaala huu, na sasa umeshakua rasmi na utatumika kwa wanafunzi wa darasa la Awali na Msingi kwa Darasa la I, III.
Aidha Mwl Neema Aliwakumbusha pia walimu kuhusu mafunzo waliyopata ya mtaala huo na kuwataka wazingatie maelekezo waliyopewa na kuhakikisha mtaala unatumika ipasavyo
“ Wote walimu wa Awali na Msingi yaani ( I, III) mmepata mafunzo ya mtaala ulioboreshwa, rai yangu kwenu ni kuhakikisha vitabu hivi pamoja na Mihtasari, inakwenda kutumika ipasavyo.
Mwisho Mkurugenzi aliendelea kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa jitihada yake ya kuboresha kwenye Elimu, lakini pia alimshukuru na kumpongeza Mhe. Jenista Mhagama Mbunge wa Jimbo la Peramiho kwa kazi nzuri anayioifanya kwenye jimbo lake, na kuhakikisha kila fulsa inayopatikana inaelekezwa kwa wananchi wa jimbo la Peramiho na Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa uju
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa