Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Ndg. Neema M. Maghembe, amewapongeza walimu wote wa Shule za msingi na sekondari, kwa mikakati waliyonayo ambaye imepelekea ufaulu mzuri wa wanafunzi ndani ya Halmashauri ya Songea.
Mkurugenzi aliyasema hayo jana katika kikao alichofanya na walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari zilizopo Halmashauri ya wilaya ya Songea. “ Matokeo ya mitihan ya utimilifu ( Mock Examination) ya darasa la saba na kidato cha nne 2023 yanamabadiliko ukilinganisha na matokeo ya mwaka uliopita na ule mwaka mwingine, kiukweli yanaonesha mabadiliko makubwa, na hii inatokana na kazi kubwa ambayo walimu mnafanya.
Mwaka huu tulikua na shule tatu katika Halmashauri yetu ambazo zimefanya vizuri sana kwa matokeo ya kidato cha sita, shule kama Peramio girls, Mpitimbi na Maposeni. Hawakuwa na division zero (0) wala division four (iv). Hii ni hatua kubwa ambayo tunapaswa kujipongeza sisi kama walimu, lakini msibweteke.
Kuhusu shule ambazo pia zimekua zikiichafua Halmsahauri kwa kutokufanya vema, Mkurugenzi alitia neno “ katika matokeo hayo hayo mazuri, zipo shule pia hazikufanya vizuri, na maafisa taaluma mpo na mnajua. sitaki kuzihukumu hapa ila natamani mjiulize afisa taaluma, na wakuu wa shule kwanini baadhi ya shule zetu hazijafanya vizuri, mje na mpango mzuri zaidi. Huwa napenda matani lakini kwenye swala la kusimamia utendaji na wajibu wetu, mtaniona mbaya. Mwaka huu hatutaki tena Songea DC turudi tulipotoka. Wakuu wa Shule tunawapa posho ya madaraka, simamieni wajibu wenu.
Mkurugenzi pia aliwatangazia habari mbaya, kwa walimu Wakuu wa shule wazembe, kwamba kipindi hiki, kila mtu arudi shuleni akazungumze na walimu wake, kuwasimamia wafanye kazi. “kipimo cha mtu kuendelea kuwa mwalimu mkuu, ni matokeo ya mtihani wa Taifa kwa wanafunzi wa mwaka huu.
Swala la miradi pia limekua agenda kwenye kikao cha mkurugenzi, kwani kuna shule ambazo zinamiradi ya Serikali, lakini kuna kutowajibika kwa baadhi ya wakuu wa Shule na Watendaji katika kusimamia miradi hiyo. Hivyo basi Mkurugenzi amewataka wakuu wa Shule wote kuhakikisha miradi ya Serikali inasimamiwa ipasavyo, na wale mafundi wazembe wote wafikishwe kwake ili awachukulie hatua.
Aidha katika kikao hicho, aliingia pia Katibu Tawala wa Wilaya, Ndg. Mtela Mwampamba, ambae pia ni mwalimu kwa taaluma ambapo pamoja na mambo mengine aliwasihi waalimu wajitahidi kusimamia taaluma zao kwa weledi, kwani Serikali inaimani kubwa na walimu.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa