Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea Ndg Neema M Maghembe amesisitiza wazazi na walezi wote wenye watoto wanaotakiwa kuanza masomo wahakikishe wanapelekwa shuleni kuanza kusoma ili kuendana na kalenda ya masomo ya mwaka 2024.
Ameyazungumza hayo wakati akitoa taarifa rasmi ya kufunguliwa kwa shule zote za Serikali katika Halmashuri ya Wilaya ya Songea na Tanzania kwa ujumla ambapo shule zote za msingi na sekondari zimefunguliwa rasmi 08 January 2024, hivyo Mkurugenzi Mtendaji amesema wanafunzi hao wanaotakiwa kuwasili shuleni kwani mazingira ni wezeshi kwa kila mwanafunzi kujifunza. Amesema
"Halmashuri ya Wilaya ya Songea ina jumla ya shule ya za msingi takribani 80 na zote zinapokea wanafunzi wa Darasa la awali na Darasa la kwanza hivyo nitoe wito kwa wazazi wote ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea kumpeleka mtoto shuleni mapema ili akaanze masomo, wala mzazi asigope kama hana sare kwani Serikali imeweka utaratibu mzuri wanafunzi wote watapokelewa bila kujali kama ana sare ya shule au Hana sare ya shule"
Vilevile Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuongeza shule katika Halmashuri ya Wilaya ya Songea hasa katika maeneo ambayo shule zilikuwa na msongamano mkubwa wa wanafunzi kwa mfano shule ya msingi Nambarapi Kata ya Kilagano, shule ya msingi Jenista iliyopo Kata ya Muhukuru, pia Shule ya sekondari Jenista Mhagama iliyopo Kata ya Parangu hivyo kupitia shule hizi mpya zimewezesha kupunguza msongamano wa wanafunzi pia kupunguza umbali mrefu wa kutembea kwa wanafunzi, vilevile ameishukuru Serikali kwa kuweka miundombinu mizuri katika shule hizo ikiwemo madawati. Hivyo amewatoa hofu wanafunzi wote ambao wanaotakiwa kuanza masomo waende wakasome kwa kuwa kuna mazingira wezeshi.
Nao baadhi ya wanafunzi wa Shule za msingi wametoa Shukrani kwa Serikali kwa mapokezi mazuri kwa wanafunzi wanaoanza na hata wale wanaoendelea wameishukuru Serikali kwa kuwaboreshea miundombinu ikiwemo Madarasa, madawati na viti. Wamesema
Stevia Mbunda mwanafunzi wa Darasa la sita Shule ya msingi Nambarapi " Tunamshukuru sana Mhe Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutujengea shule nzuri ina madawati, Madarasa ya kutosha nasi tunamuahidi kusoma kwa bidii"
Yakobo Mwenda mwanafunzi wa Shule ya msingi Mgazini amesema" tunawashukuru sana wazazi wetu kwa kutununulia sare za shule, wametulipia chakula nasi sasa tunakila shuleni, pia Tunamshukuru sana Serikali kwa kutulipia ada kwa upendo huo nasi tunaahidi kufaulu katika masomo yetu"
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa