Mkugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Bi Neema Maghembe amekabidhi vyumba vya madarasa 65 vilivyojengwa kupitia Mpango wa maendeleo kwa ustawi waTaifa na mapambano dhidi ya UVIKO -19 kwa Mkuu wa Wilaya Songea Pololet Mgema.
Maghembe amefafanua katika vyumba hivyo,vyumba 46 ni kwa ajili ya Sekondari zote 16,ambavyo vimegharimu jumla ya Shilingi milioni 920 na vyumba 19 vimejengwa kwenye vituo shikizi vitano vya Shule za Msingi ambavyo vimegharimu Shilingi milioni 320.
“Watoto wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2022 wataanza masomo kama ilivyopangwa”,amesema Maghembe
.
Akipokea vyumba hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema amewapongeza viongozi na wadau waliofanikisha kazi hiyo na kuwataka kuendelea kusimamia vema miradi inayoendelea kutekelezwa katika maeneo yao.
Mgema amesema vyumba vilivyojengwa vinakwenda kutatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika Shule za Msingi na Sekondari na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia,hivyo umakini mkubwa unatakiwa katika kulinda miundo mbinu hiyo.
Serikali imetoa bilioni 1.3 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 65 katika Halimashauri ya Wilaya ya Songea
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa