• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

MKOA wa Ruvuma unahazina ya makaa ya mawe tani 227

Tarehe ya Kuwekwa: October 16th, 2020

Shughuli za utafiti na uchimbaji wa makaa ya mawe katika mkoa wa Ruvuma zinafanyika katika Wilaya ya Mbinga maeneo ya Mbalawala na Mbuyula, Wilaya ya Songea katika maeneo ya Muhukuru, Njuga na Mtyangimbole na Wilaya ya Nyasa maeneo ya Malini kata ya Mtipwili na Mbambabay.

Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Jumanne Mohamed Nkana amesema Mkoa wa Ruvuma una hazina ya makaa ya mawe zaidi ya tani milioni 227 ambayo yanatarajiwa kuchimbwa kwa miaka 300.

Kulingana na Nkana,tafiti za awali za makaa ya mawe zimefanyika katika maeneo ya Mbalawala Mbinga ambako imebainika kuwa na tani milioni 99.5, Mbuyula Mbinga tani milioni 15.1 na Muhukuru Songea tani milioni 27.

Kwa mujibu wa Nkana tafiti katika eneo la Njuga wilaya ya Songea kuna tani milioni 23, wilaya ya Nyasa maeneo ya Malini tani kata ya Mtipwili milioni 29, kijiji cha Liweta Kata ya Mbaha tani milioni 34.Amesisitiza kuwa ubora wa makaa ya mawe yanayopatikana kwenye maeneo hayo yana wastani wa Calorific Value (CV)5,000 hadi 7,000.

Hata hivyo Afisa Madini Mkazi huyo wa Mkoa wa Ruvuma amesema uchimbaji mkubwa wa makaa ya mawe unafanyika katika maeneo ya Mbalawala,Mbuyula, Mbambabay, Muhukulu na Liweta.

Amewataja wateja wakubwa wa makaa ya mawe yanayochimbwa katika maeneo hayo kwa sasa kuwa wapo ndani ya nchi na katika nchi jirani za Rwanda, Kenya na Uganda na kwamba wanatarajia kuanza kuuza makaa ya mawe katika nchi ya India.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ameziagiza kampuni zinazochimba makaa ya mawe mkoani humo kuuza makaa ya mawe kwenye viwanda vya ndani ili kupata nishati ya kutosha na ziada inayobaki isafirishwe kwenda nje ya nchi.

Mndeme pia ameziagiza Kampuni hizo kutoa ajira kwa Watanzania ili waweze kunufaika na rasilimali za nchi huku akisisitiza kuchimba makaa ya mawe yenye viwango ili soko lipanuke, na kuzingatia usalama na afya za watumishi wote wanaofanya kazi katika migodini.

Maamuzi ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli Kuzuia kuagiza makaa ya mawe toka nje,badala yake watumiaji wote kutumia makaa ya mawe ndani ya nchi,hususani toka Mkoani Ruvuma, kumesababisha soko la makaa hayo kupanda na kutoa ajira kwa watanzania.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Oktoba 15,2020

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAAFISA HABARI KIMEMALIZIKA KWA KUWEKA MAKUBALIANO ENDELEVU KWA MASLAHI MAPANA YA NCHI

    May 24, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA, WANATEGEMEA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA NA UBINGWA BOBEZI KATIKA HOSPITALI YA HALMASHAURI SONGEA

    May 21, 2025
  • MKIMBIZA MBIO ZA MWENGE KITAIFA, AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    May 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SONGEA DC, LIMEMSHUKURU MHE. RAIS NA WAZIRI WA AFYA KWA KUIHESHIMISHA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    April 29, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa