Mji mdogo wa Peramiho katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wote kurasimishwa kwa lengo la wananchi wapate haki yao ya kumiliki maeneo yao kisheri na kuupandisha hadhi kutoka kwenye Kijiji kwenda kuwa Mji.
Afisa ardhi wa Halmashauari hiyo Godfrey Chipakapaka amesema pamoja na lengo la kuupandisha hadhi mji huu,lengo jingine ni kuwataka wananchi kulipa kodi ya ardhi baada ya taratibu zote za upimaji na umiliki kukamilika.
Chipakapaka amesema urasimishaji wa mji huu unafanywa na Serikali kwa kushirikiana na shirika l silo la kiserikali la Aga Teo Hope Foudandation (AHP) kwa gharama za shilingi 150,000 gharama ambyo ni kidogo sana ukilinganisha na gharama halisi za upimaji ambazo mwananchi ataamua kulipa mara moja au kidogo kidogo kwakipindi cha miezi miwili.
“Upimaji huo ni fursa kwa wananchi hivyo wanapaswa kuchangamkia kwasababu gharama inayotumika katika kupima ni ndogo, kisheria kupima uwanja wa robo hekali ni sh.600000”,amesema Chipakapaka
Mratibu wa Shirika la Aga Teo Hope Foundation William Mapunda amesema kazi ya upimaji wa viwanja hivyo umeshirikisha wananchi kwa wao kuunda kamati ambayo inaratibu zoezi zima ikiwemo utambuzi wa mipaka na usimamizi wa malipo ambayo wanalipia Bank..
“Tunashukuru Ofisi ya Kamisha wa Ardhi wa Mkoa wa Ruvuma kwakuona umuhimu wa kazi hii kwakutupatia kifaa cha kisasa cha kupima ardhi kichotumia sateliti ambacho kinapima ardhi kiliomita 30”,alisema Mapunda.
Ameongeza kwa kusema wanatarajia kupima viwanja 5260 katika Mji mdogo wa Peramiho ambapo kazi hiyo imeshaanza mwezi wa huu Septemba na upimaji utakamilika mwezi Desemba mwaka huu,sambamba na upimaji wa mji mdogo wa Peramiho maeneo mengine ambayo wanatarajia kupima ni Parangu,Litisha,Kilagano,Liganga na Mbinga mhalule.
Afisa Mipango miji wa Halmashauri ya Wilaya Medradius Aliyafao amesama lengo la serikali ya mkoa wa Ruvuma ni kupima viwanja 7000 kwa mwaka lakini kwa Halmashauri hiyo itatavuka lengo la upimaji hadi kufikia mwezi Desemba 2020.
Aliyafao amesema ardhi ni mtaji zoezi la urasimishaji litawasaidia wananchi kukopa fedha toka kwenye Taasisi za kifedha,fedha ambazo zitawasaidia kufanya shughuri nyingine za kiuchumi kama kiliomo, ufugaji,uvuvi na biashara.
“Naona miujiza kwani nimuda mrefu tumekuwa na kilio cha kupiwa maeneo yetu na kupatiwa hati’,amesema Maria Ponera.
Maria Ponera ambaye ni mkazi wa kijji cha Peramiho B amesema wanashukuru Serikali na shirika la Aga TEO Hope Foundation kwasabu kitendo cha kupiwa maeneo yao na kumilikishwa kisheria kilikuwani kilio chao cha mda mrefu kwa wakazi wa Peramiho jambo ambalo litamaliza migogoro ya mipaka ya viwanja na mashama ambayo ilikuwa inajitokeza miongoni mwao kwasasa hali hiyo itakwisha kwani kila mtu atatambua mipaka ya eneo lake,pamoja na kukopesheka kwenye mabenki kwa kuweka dhamana ya hati zao Imeandaliwa na
Jacquelen Clavery,
Afisa Habari Songea DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa