UKAGUZI WA MIRADI
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh Christina Mndeme ametembelea na kukagua miradi mbali mbali itakayo zinduliwa,kufunguliwa na kuwekewa mawe ya msingi na Mwenge wa uhuru mwaka 2018 katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Ametembelea na kukagua miradi hiyo katika kata za Liganga,Mbingamhalule na Magagura na kuridhishwa na hatua za miladi hiyo hivi karibuni.
Miradi itakayo funguliwa ni madarasa na choo,nyumba ya mwalimu na mashine ya kusindika mahindi,mradi utakao zinduliwa ni shamba la umwagiliaji kwa matone na mingine itakaguliwa.
Mwenge wa uhuru unatarajia kupokelewa na kukimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea juni 6 mpaka juni 7 na baadaye kukabidhiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kilomita 118 ndani ya Halmashauri hatimaye kupokelewa na Halmashauri ya Manispaa ya Songea eneo la Sinai na kufanya jumla ya kilometa 189 zitakazo kimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Aidha Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Songea Bw Simon Bulenganija anatoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika maeneo ambayo mwenge wa uhuru utapita na yale ambayo hautapita kuungana pamoja kuupokea,kuukimbiza na kuuushangilia mwenge wa uhuru
IMETAYARISHWA NA JACQUELEN CLAVERY.KITENGO CHA
HABABARI MAWASILIANO NA MAHUSIANO KAZINI-14/05/2018
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa