Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza zoezi la utambuzi ,usajili na ufuatiliaji wa mifugo kwa njia ya heleni za kieletroniki kwa lengo la kutambua idadi ya mifugo nchini, kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi na kurahisisha mipango ya kuihudumia.
Hayo ameyasema Afisa Mifugo na Uvuvi wa Halamashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Dr Erick Kahise akiwa Ofisini kwake.
Dr Kahise amesema katika utekelezaji wa zoezi hilo Serikali imetoa Mwongozo ambao unaelekeza watu binafsi kuingia makubaliano na Serikali ili waweze kusambaza na kuvisha mifugo heleni za kieletroniki kwa usimamizi wa Halmashauri za Wilaya
Dr Kahise amezitaja faida za usajili wa kieletroniki ni pamoja na kutambua idadi ya mifugo na sehemu ilipo,kukabiliana na changamoto ya magonjwa ya milipuko ambayo pia ni tishio kwa uhai wa binadamu,urahisishaji wa biashara ya mifugo na mazao yake,uthibiti wa wizi pamoja na kuwawezesha wafugaji kupata mikopo na bima.
Dr Kahise amesema katika utekelezaji wa zoezi hilo Serikali imetoa Mwongozo ambaoa unaelekeza watu binafsi kuingia makubaliano na Serikali ili waweze kusambaza na kuvisha mifugo heleni za kieletroniki kwa usimamizi wa Halmashauri za Wilaya
Ameitaja mifugo itakayo husika na zoezi hilo kuwa ni ng’ombe , punda, kondoo na mbuzi wenye umri zaidi ya miezi mitatu wanaofugwa kwenye mashamba ya serikali,Ranchi, mashamba ya watu binafsi na mifugo iliyopo kwenye maeneo yote ya unenepeshaji,wanaopelekwa mnadani na machinjioni na wanaosafirishwa toka eneo moja kwenda jingine.
Dr Kahise amewataja wadau mbalimbali watakao husika na usimamizi na ufuatiliaji wa zoezi hilo kuwa Serikali za Vijji,watoa huduma binafsi na wafugaji wenyewe kwa kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za nchi.
Ameongeza kwa kusema heleni ambazo zitawekwa kwenye mifugo hiyo zitakuwa zina fanana isipokuwa kuwa Kwa Wilaya ambazo zipo mipakani mwanchi heleni hizo zitatofautiana rangi kwa lengo la kudhibiti changamoto mbalimbali ikiwemo ya wizi wa mifugo.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery.
Afisa Habari
Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa