Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI (ELIMU) Mhe. Zainab Katimba amewata Watumishi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa wanaoshiriki mashindano ya SHIMISEMITA 2025 kutumia mashindano hayo kama sehemu ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la upigaji kura wa kuchagua Rais Wabunge na Madiwani siku ya Oktoba 29, 2025.
Mhe Zainab ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mashindao ya SHIMISEMITA leo Agosti 23, 2025 katika Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.Mhe. Katimba amewataka watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kushiriki kikamilifu mashindano haya na kuwakumbusha wananchi kuhusu zoezi kubwa la kitaifa la uchaguzi ikiwa ni sambamba na kuwaelimisha wananchi
"Kupitia kauli mbiu hiyo Sanaa na Michezo ikawe chachu ya watumishi wengine ambao hawakupata fursa hii na jamii kwa ujumla kuonesha uzalendo wa kuipenda nchi yao kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, 2025 na kuchagua viongozi walio bora na siyo bora viongozi" amesema Mhe. Katimba.
Katika Hotuba yake Mhe. Katimba amethibitisha kuwa jumla ya Halmashauri 150 kati ya 184 zimeshiriki na jumla ya Watumishi walioshiriki Mashindano ni 3504 ambapo Wanawake ni 1390 na Wanaume 2114
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa