MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya Songea Mhe. Menasi Komba leo Septemba 28,2022 mbele ya mkuu wa wilaya Mhe.Pololet Mgema, Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Neema Maghembe, Viongozi wa Chama na Wataalamu wamepokea taarifa ya hesabu za Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2022.
''Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Neema Maghembe na watendaji wote kwa jinsi walivyoweza kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kwa asilimia 123.5 kwa mwaka wa fedha 2021/2022'', amesema Mhe.Menasi Komba
Akisoma taarifa hiyo muhasibu wa Halmashauri Viviano Ndunguru amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya fedha ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 kifungu cha 40 kama ilivyorekebishwa mwaka 2000 Halmashauri zote nchini zinatakiwa kufunga hesabu na kuwasilisha kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za seikali (CAG) si Zaidi ya tarehe 30 september kila mwaka.
Aidha Viviano amesema kuwa kazi ya ufungaji wa hesabu kwa mwaka 2021/2022 ilianza tarehe 10 Julai na imekamilika tarehe 25 sept 2022
Imeelezwa kuwa Mfumo wa ufungaji wa hesabu kimataifa ujulikanao kama ipsus ndio uliotumika katika uandaji wa hesabu za halmashauri ya wilaya ya songea pia katika mwaka wa fedha 2021/2022 hesabu zimetolewa katika mfumo wa muse kama muongozo wa ufungaji hesabu unavyotaka ambao ni mfumo wa taifa la Tanzania.
Naye Diwani wa kata ya Liganga iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mhesimiwa Filbert Mendrad Soko amesema kuwa taarifa hiyo wao kama Madiwani wameipokea vizuri kwani imekidhi matakwa ya baraza katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kusisitiza juhudi zilizofanyika katika awamu hii ziendelee Zaidi katika mwaka wa fedha ujao.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Septemba 28, 2022.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa