Mbunge wa Jimbo la Peramiho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Joakim Mhagama ameendelea na Ziara Katika Kata ya Parangu Kijiji Cha Litowa.
Katika Ziara hiyo ameambatana na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Waheshimiwa Madiwani pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo.
Mheshimiwa Mbunge alianza kushiriki Misa takatifu katika kanisa lililopo kijiji cha Litowa.
Aidha, katika ziara hiyo Mheshimiwa Jenista amegawa Viti saba vya kutembelea wagonjwa(wheel chair), Mashuka, Mablangeti, Vifaa vya Kujifungulia akina Mama, Nguo za Watoto Wachanga pamoja na Vifaa vya Michezo (Jezi na Mipira) Kwa Timu Za Mpira Tatu za Kijiji Cha Litowa.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa