Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama amewataka wazazi kulinda watoto dhidi ya uwazi na utandawazi ambao unaharibu mila, desturi na maadili.
Ameyasema hayo katika mkutano wa adhara uliofanyika katika kijiji cha Litowa Kata ya Parangu.
“Unyanyasaji wa watoto umeongezeka sana zamani tulikua tunaangaika kulinda watoto wakike lakini sasa hivi hadi watoto wadogo wakiume wananyanyasika zaidi wanafanyiwa vitendo vya kikatili hivyo nawasihi wazazi wenzangu tuwe karibu na watoto kwa kuangalia tabia na mienendo yao kila siku”, amesisitiza Mhe. Jenista.
Aidha, Mheshimiwa Mbunge ametoa wito kwa wananchi kuunga mkono juhudi na jitihada za Serikali za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanaume, wanawake na watoto hivyo amewataka wazazi kulinda watoto ili wawe salama.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa