Kikao cha baraza la madiwani robo ya pili Halmashauri ya Songea kimefanyika januari 31 katika ukumbi wa Halmashauri kikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani wote wa Halmashauri hiyo, watendaji wa kata pamoja na wageni waalikwa.
Mhe. Saimoni kapinga ambaye ni Diwani wa kata ya Lilahi na pia ndio makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilayay ya Songea, pamoja na Mambo mengine alisisitiza ushirikiano kati ya Madiwani na wataalam ili kuendelea kulijenga Taifa
Katika kikao hicho kamati mbalimbali ziliwasilisha taarifa zao na kamati hizo ni pamoja na kamati ya Maadili, Fedha, kamati ya Uongozi na Mipango ,kamati Kudhibiti Ukimwi, kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira,na kamati ya Elimu Afya na Maji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi Neema Magembe amesema kuwa baraza limejadili taarifa mbalimbali na zimepitiwa na kuongeza kuwa inatakiwa kuwekea mkazo kama menegmenti na kuzifanyia kazi kikamilifu na kuendelea kuchapa kazi.
Aidha Bi neema aliendelea kuwapongeza Wataalmu wake ( wakuu wa Divisheni na Vitengo) kwa kazi nzuri ambazo wamekua wakifanya, huku akisistiza uwepo wao na utendaji kazi wao ndio unaoifanya Halmashauri kuendelea kusemwa vizuri nje.
Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea Mhe, Simon Kapinga amewahasa madiwani kuwahamasisha wananchi kulima zao la ufuta kwa wingi kwani ni zao ambalo lina mpa mkulima fedha ya mapema sana na kuondokana na matatizo ya kiuchumi.
"Niwahase madiwani wenzangu mhakikishe mnawahamasisha wananchi walime zao la ufuta hasa kwa kipindi hiki cha mwezi huu wa pili kwasababu ni zao linalo wapatia hela mapema na kuwasaidia katika majukumu mengine"
Amesisitiza Kapinga
Hata hivyo Mhe. Mwenyekiti amewataka watendaji wa kata kuhakikisha wanawahimiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto ambao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na kuacha kuwapa watoto ajira za utoto.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa