MBUNGE wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Sera,Bunge,ajira,vijana na wenye ulemavu Bi. Jenista Mhagama jana ametunukiwa heshima ya kuwa malkia wa nguvu wa kabila la wangoni ili kuenzi shughuli anazofanya za kuleta maendeleo kwenye Jimbo hilo toka amechaguliwa kuwa mbunge .
Awali akimtunukia heshima hiyo ya umalkia chifu wa kabila la wangoni Emanuel Zulu kwenye eneo lililokuwa kambi ya Wajerumani kwaajiri ya kupumzikia lililopo katika kijiji cha Namatuhi Wilaya ya Songea.
Alisema kuwa Bi. Jenista amefanya kazi kubwa iliyotukuka ya kuwaletea maendeleo katika sekta ya Elimu ambapo ameweza kujenga na kuboresha miundombinu ya majengo katika shule za msingi na sekondari,
Alifafanuwa kuwa katika sekta ya Afya aemeweza kujenga zahanati na vituo vya afya na kufanya huduma hizo kutolewa kwa ubora ,lakini pia ameweza kuboresha miundombinu ya barabara katika kiwango cha rami kwenye vijiji vyote vya halmashauri ya wilaya ya Songea.
''Najuwa watu wanaweza kushangaa kwa nini tumempa umalkia tumeamua kumpaa umalkia baada ya yeye kulifahamu vizuri jimbo la peramiho na amekuwa na utamaduni wa kushinda na wananchi jimboni kwake hivyo aina utofauti na nchi zingine kama Misri waliweza kumsimika umalkia Cleopatra hata kwa sisi kumuhenzi"alisema Chifu Zulu.
Alisema wapo wabunge wengi wamepita na wamefanya kazi nzuri lakini huyu amefanya kazi nzuri zaidi inayoonekana kwa jamii ukizingatia kuwa Rais wa Jamuhuri ya Munngano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amemwamini kwa kumpa majukumu makubwa ambapo wananchi wanajivunia.
Kwa upande Mbunge Jenista Mhagama ameshukuru kupewa heshima kuwa malkia wa nguvu kwa jimbo la peramiho na kwamba ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma ikiwemo kwa wananchi wa jimbo la Peramiho.
Alisema kuwa serikali kupitia Wizara ya afya imeshatoa zaidi ya sh. milioni 500 kwaajiri ya ujenzi wa kituo cha afya ambacho kinatarajiwa kujengwa katika kata ya Mpitimbi hivyo na kufanya idadi ya vituo vya afya visivyopungua vitano.
Aidha amewataka wananchi kuona umuhimu wa kulima mazao mbadala badala ya kutegemea kilimo cha zao la mahindi ambalo kwa sasa soko lake limeyumba wakati serikali inaendelea na jitihada za kutafuta soko la mahindi.
MWISHO.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa