MBUNGE AHAIDI NEEMA KWA WAKULIMA JIMBONI KWAKE
Mbunge wa Peramiho ambaye pia ni Waziri wa chi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Joakim Mhagama, amewaahidi wananchi wa Jimbo la Pramiho kupata mbole ya rukuzu kwa bei nafuu, na itawafikia wote kwenye kata mpaka vijiji vyote vilivyopo jimboni kwake.
Mbunge ameyasema hayo, wakati akifanya ziara yake ya siku nne 18/09/2023 mpaka 21/09/2023 katika kata ya Kilagano, Mpitimbi, Matimila na Magagura. Mbunge aliwataka wananchi wasiwe na hofu na serikali yao, kwani Serikali ipo makini kuhakikisha kila mwananchi anapata haki zote za msingi ili kurahisisha shughuli yao zinazowaingizia kipato ikiwemo kilimo.
“Hapo mwanzo swala la mbolea kwa wakulima ilikua mtihani sana, kwanza ilikua inauzwa bei kubwa ambapo ni kuanzia 130,000 mpaka 120,000. Lakini kwa sasa inapatikana kwa shilingi elf sabini tu, (70,000). hili swala lazima tumpongoze Rasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa upendo wake kwa wananchi, na niwaambie tu mikakati wake ni kwamba mwaka huu mbolea zote zinafika katika kila Kata, na kila kijiji ili kila mkulima aweze kupata mbolea kwa urahisi na kwa bei nafuu.”
Mbunge alitoa onyo kwa mawakala wa Mbolea kwa kuwataka wamalize taratinbu zao zote mapema na pia kutokulifanya hili swala la mbole kama sehem ya kuwanyanyasa wananchi. Hivyo aliwataka waache udanganyifu na kumuunga mkono Mhe. Rais ili kufikisha adhima yake ya kurahisisha maisha kwa wananchi wake.
“ Mawakala wa mbolea simamieni hili swala kwa weredi, epukeni udanganyifu na zoezi hili lianze mapema kwan litawasaidia wananchi kupata mbolea mapema na kufanya kilimo kwa wati.”
"Wananchi sasa Serikali yenu ya awamu ya sita ipo kwa ajili ya kuwahudumia ninyi na kuwapa kile ambacho kinarahisisha maisha ya kila mtanzania ikiweno ninyi watu wa Jimbo la Peramiho. Hivyo nawaomba mkajisajili mapema, ili mbolea zinatakapofika mpate kwa wakati na kazi iendelee"
Mh mbunge pia alipongeza jitihada za serikali kwa kuleta huduma za kijamii na miundombinu yote muhimu katika vijiji vyote kama vile Maji, Barabara ujenzi ma wadarasa, majaraja na Umeme. Lakini pia aliwasauri wananchi kutumia fulsa zilizopo kujiongezea kipato.
“ tumieni fulsa mnazozipata kwa maendeleo yenu, saivi kila kijiji kina umeme, ambavyo bado mmeona hapa nipo na wataalamu kutoka Tanesco na wataalam wengine ikiwemo Tarula na Rea hivyo vijiji vyote vyenye changamoto zitatatuliwa. Hivyo tuanze kujiajili kupitia umeme kwa kutengeneza Saluni, Kuchomelea ili kuutumia umeme uliopo kama fursa.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa