Msimamiwa wa uchaguzi wa jimbo la Peramiho Simon Bulenganija ametoa onyo kwa mawakala wa vyama vya siasa watakaojitoa ufahamu kwa lengo la kuvuruga uchaguzi mkuu mkono wa sheria hautawaacha salama.
Bulenganija ametoa onyo hilo kwa nyakati tofauti wakati akiwaapisha kiapo cha kutunza siri mawakala wa vyama vya siasa ambao wameteuliwa na vyama katika Mji mdogo wa Peramiho na Kijiji cha Mpitimbi katika Jimbo la Peramiho Mkoani Ruvuma.
Amesema kwa wakala yeyeto atakayejito ufahamu kwalengo la kuvulruga uchaguzi mkuu, siku ya uchaguzi Oktoba 28, 2020 iwe,wakati wa kupiga kura, kuhesabu kura,kujumlisha kura na kutangaza matokea mkono wa sheria hauta muacha salama kwasababu zoezi la uchaguzi lipo kwamujibu wa kanuni taratibu na sheria za Nchi.
“Lazima mpime vizuri kazi ya kusimamia maslahi ya chama lakini pia umuhimu na ulazima wa kuzingatia sheria,kanuni,taratibu na maelekezo ya Tume”,alisema Bulenganija.
Amewataka mawakala kila wakala kutimiza jukumu alilopangiwa na kuacha kuingilia jukumu ambalo wakala hakupangiwa katika kipindi cha kupiga kura,kuhesabu kura kujumlisha kura na kutangaza matokeo.
Bulenganija ameongeza kwakusema vyama ambavyo havijawasilisha orodha ya majina ya mawakala wa vyama vyao katika Ofisi ya Msimamizi wa jimbo la Uchaguzi hawataruhiswa kusimamia uchaguzi kwamujibu wa maelekezo ya Tume,ambapo katika jimbo hilo vyama viwili tu ambavyo vimetimiza sharti hilo ambavyo ni Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Amewakumbusha wanachi wote wenye sifa na vigezo kujitokeza kwa wingi kwenda katika vituo vyao walivyojiandikisha kwenda kupiga kura ifikapo siku ya jumatano Oktoba 28,2020 pasipo na shaka yoyote kwani Tumeya Uchaguzi imeimarisha ulinzi ili kuhakikisha kila mtu anapiga kura kwa uhuru.
Amesema maandalizi yote ya zoezi la uchaguzi yanaenda vizuri na tayari Tume ya Taifa ya uchaguzi imeshafikisha vifaa kwa asilimia 98 ambavyo vinatakiwa katika kufanikisha zoezi hilo.
Kwaupande wake Msimamizi msaidizi wa Jimbo la uchaguzi Kangese Masanja amesema mawakala ni kundi la watu muhimu katika kufanikisha zoezi la uchaguzi ,hivyo nivema wakazingatia maelekezo yote yanayotolewa naTume na kujiepusha na udanganyifu wawapo katika vituo vya kupigia kura na kuwasiliana na msimsmizi mkuu wa kituo ambaye amepewa mamlaka na Tume ya kuwa mkuu wa kituo
Jimbo la Peramiho lina Kata 16,Vijiji 56,vituo vya kupigia kura 252 na jumla ya mawakala 509 waliapa kiapo cha kutunza siri nakutotoa siri na kukiuka sheria ya kiapo adhabu yake ni kushughulikiwa na vyombo vya dola.
Ikumbukwe kwamba uchaguzi wa mwaka huu ni uchaguzi wa sita tangu Nchi ya Tanzania iingie kwenye mfumo wa vyama vingi mwaka 1992
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery-Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa