• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

MAKAMU wa Rais kuanza ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Ruvuma

Tarehe ya Kuwekwa: July 19th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Philipo Isdory Mpango anatarajia kuanza ziara ya kikazi  mkoani Ruvuma kuanzia Julai 20,2023 hadi Julai 24,2023.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake mjini Songea Kanali Thomas amesema Julai 20,2023 majira ya 5.00 asubuhi Mheshimiwa Makamu wa Rais anatarajia kuwasili katika Kijiji cha Lilondo Halmashauri ya Madaba na kupokewa na viongozi wa Chama na Serikali kisha kuwasalimu wananchi.

Amesema Makamu wa Rais akiwa katika Halmashauri ya Madaba pia atasalimiana na wananchi Kijiji cha Mlilayoyo kisha kuondoka kuelekea Ikulu Ndogo mjini Songea.

“Mheshimiwa Makamu wa Rais akiwa Ikulu Ndogo Songea atapokea taarifa ya shughuli za maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma Pamoja na kukabidhiwa taarifa ya Mkoa ya kazi za Chama Cha Mapinduzi’’,alisema.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mheshimiwa Makamu wa Rais Julai 21,2023 ataanza ziara yake katika Manispaa ya Songea ambapo atazindua kituo cha Afya Lilambo na kuwasalimia wananchi.

Amebainisha zaidi kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais ataondoka Lilambo na kuelekea  katika Kijiji cha Matomondo Halmashauri ya wilaya ya Songea ambako ataweka jiwe la msingi,Barabara ya kiwango cha lami ya  Matomondo hadi Mlale JKT yenye urefu wa kilometa 4.5,kisha atasalimiana na wananchi na kuelekea hospitali ya Peramiho ambako atafungua jengo la kusafishia figo na kukagua jengo la upasuaji na kusalimiana na wananchi.

Kulingana na Mkuu wa Mkoa,ziara ya Makamu wa Rais mkoani Ruvuma itaendelea Julai 22,2023 kwa Mheshimiwa Makamu wa Rais kushiriki katika kuzindua kampeni ya kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Kampeni hiyo inatarajia kufanyika kwa siku kumi kisha kuendelea hadi Desemba 2023.Kampeni hiyo inatarajia kufanyika katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma ambapo kila Halmashauri kampeni itafanyika katika kata kumi

Hata hivyo amesema baada ya uzinduzi huo Mheshimiwa Makamu wa Rais  atakwenda Kata ya Mwengemshindo Manispaa ya Songea kukagua ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa na kuzindua jengo la mionzi la hospitali ya Rufaa ya Mkoa.

Kanali Thomas amebainisha kuwa Julai 23,2023 Mheshimiwa Makamu wa Rais ataendelea na ziara yake mkoani Ruvuma kwa kutembelea wilaya za Mbinga na Nyasa na kwamba akiwa wilayani Mbinga katika Kijiji cha Kigonsera,Makamu wa Rais atasalimiana na wananchi wa Kigonsera na kisha Kwenda Mbinga mjini ambako atasalimiana na wananchi wa Mbinga mjini.

Amesema Makamu wa Rais ataondoka mjini Mbinga na kuelekea mji Mdogo wa Mbambabay wilayani Nyasa ambako anatasalimiana na wananchi kisha kuondoka na kuelekea Kijiji cha Liuli  ambako ataweka jiwe la msingi katika mradi wa maji safi Liuli na kusalimiana na wananchi wa Liuli.

“Natoa rai kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika maeneo yote ambayo Makamu wa Rais atapata fursa ya kuwasalimia wananchi’’,alisema.

Mheshimiwa Makamu wa Rais anatarajia kukamilisha ziara yake mkoani Ruvuma Jumatatu Asubuhi  Julai 24,2023.

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAAFISA HABARI KIMEMALIZIKA KWA KUWEKA MAKUBALIANO ENDELEVU KWA MASLAHI MAPANA YA NCHI

    May 24, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA, WANATEGEMEA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA NA UBINGWA BOBEZI KATIKA HOSPITALI YA HALMASHAURI SONGEA

    May 21, 2025
  • MKIMBIZA MBIO ZA MWENGE KITAIFA, AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    May 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SONGEA DC, LIMEMSHUKURU MHE. RAIS NA WAZIRI WA AFYA KWA KUIHESHIMISHA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    April 29, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa