Mahitaji ya chanjo ya UVIKO -19 yazidi kuongezeka katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma baada ya wananchi kupokea elimu ya umuhimu wa chanjo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Geofrey Kihaule amesema mahitaji ya chanjo yanamezidi kuongezeka baada ya wananchi kuendelea kujitokeza kwawingi katika vituo vya kutolea huduma za afya wakihitaji kuchanja chanjo ya UVIKO-19 kwa lengo la kujikinga na ugonjwa huo
“wananchi wengi wamehamasika kuchanja ,na mahitaji ya chanjo bado ni makubwa “amesema Kihaule.
Dr Kihaule amewatoa hofu wananchi kuendelea kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya na kupata chanjo kwasababu chanjo zipo na zitaendelea kuletwa.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
A/Habari Songea DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa