Kati ya Maghala ya chakula Ishirini na nane (28), yatakayojengwa Mkoani Ruvuma, Maghala kumi na moja ( 11) yatajengwa Halmashauri ya wilaya ya Songea katika kata mbalimbali ikiwemo Peramiho, magagula nk Maghala tisa yatajengwa wilaya ya Madaba, Maghala saba wilaya ya Namtumbo na moja Wilaya ya Songea Mjini.
Hayo yalisemwa jana kwenye ziara ya Mhe. Jenista Mhagama katika kata ya Magagura ambapo alimbelea maghala mawili, moja kati ya hayo ndo lilikua linaanza ujenzi.
Akitoa ufafanuzi kwa wandishi wa habari Mkandarasi wa jengo hilo Eng. Julius Nalitolela alisema “ hili ni ghala hapa Masangu, ni kati ya maghala kumi na moja yanayojengwa katika Halmashauri ya wilaya ya Songea, pia kati ya maghala 28 yaliyopo Mkoa wa Ruvuma. Mradi huu unaghalimu kiasi cha shilingi Milioni mia tano ishirini ( 520,000,000.00) ni Mradi ambao utaweza kuhifadhi vyakula mbalimbali kiasi cha Tani elfu moja ( 1000) na litakua na ukubwa wa Squre meter mia tano sitini ( 560) ambalo pia itakua na ofisi na vyoo kwa ajili watumishi.
Akikagua Ghala hilo Mhe. Jenista aliwataka viongozi na wasimamizi kuwapatia nafasi wazawa katika kazi ndogondogo za pale ili waweze kujipatia kipato, pia akashauri hata kandarasi ndogo ndogo ziweze kupewa kwa wazawa ili kukuza uchumi wa kijiji cha Masangu.
“ kwanza niwapongeze Halimashauri kwa kusimamia vema miradi ya serikali, nikupongeze Mkurugenzi Neema Maghembe na timu yako nzima, lakini nishauri pia vipaumbele vya ajira viwe kwa wazawa, ili waweze kujipatia kipato kutokana na vitu vinavyofanyika kwenye maeneo yao ikiwemo pia kupewa kandarasi ndogo ndogo wazawa wa hapa hapa kijijini. Natoa wito pia kwa wanakijiji kuwa walinzi wa mali za Serikali"
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa