Afisa Mwandikishaji Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bi. Elizabeth M. Gumbo jana 09/01/2025 alifungua semina ya mafunzo kwa watendaji ngazi ya Kata kwaajili ya Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura
Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza jana tarehe 9/1/2025 yanatarajiwa kuhitimishwa leo tarehe 10/1/2025 katika ukumbi wa Jenista Muhagama Maposeni Sekondari.
Akifunga mafunzo hayo Afisa mwandikishaji jimbo la Peramiho amewasihi watendaji hao kutunza kiapo chao cha uaminifu na kutunza siri pamoja na kuhakikisha wanatumia vyema mafunzo hayo ili wakawahudumie ipasavyo wananchi na kufanikisha malengo ya zoezi hilo kama ilivyokusudiwa.
“Serikali imegharamikia mafunzo hayo ili kuwawezesha ninyi ujuzi ambao utaenda kusaidia katika kuhakikisha zoezi hili linaenda kikamilifu, niwasihi sana mheshimu kiapo, mkatunze siri ikiwa ni sehemu ya kiapo chenu lakini pia mkafanikishe malengo ya zoezi hili kama ilivyokusudiwa.
Zoezi hilo la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linatarajiwa kwanzia tarehe 12/1/2025 na kumalizika tarehe 18/1/2025 ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa