Mafunzo hayo kwa maafisa Mipango, Wahasibu, Maasifa Tehama, Waganga wakuu wa Halmashauri na Makatibu wa Afya wa Halmashauri yanaendeshwa na Ofisi ya Rais Tamisemi chini ya ufadhili wa PS3. PS3 ni shirika la kimarekana linalofadhili miradi ya uboreshwaji wa sekta za umma. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Mtwara kuanzia tarehe 24 Julai mpaka 31 julai 2017.
Mfumo wa Planrep ulioboreshwa utatumika katika uandaaji wa bajeti za Halmashauri zote nchini pamoja na kuzituma bajeti hizo katika ngazi za wizara kwa ajili ya utekelezaji.
Uwepo wa mfumo huo utasaidia kupunguza gharama za uchapishaiji wa bajeti pamoja na kurahisha utumaji, upokeaji wa taarifa na kupunguza muda wa kuandaa bajeti.
Mfumo huo ni rahisi kuutumia na utapatikana kupitia njia ya tovuti na utahifadhiwa katika komputa kuu Tamisemi Dodoma.
Mfumo wa FFARS unalenga kurekodi na kutunza taarifa za fedha zinazopelekwa moja moja katika akaunti za Zahanati na Shule ili kujua matumizi ya fedha hizo katika ngazi ya vituo vya kutolea huduma.
Baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo wataalamu hao wanatakiwa kuwawezesha watumishi wenzao ili waweze kuitumia mifumo hiyo kwa ufanisi.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa