Maelfu ya wananchi wa Jimbo la Peramiho wajitokeza kumuona Dkt. Samia
Dkt. Samia, ametembelea jimbo la peramiho leo 24/09/2024 na kuzungumza na wananchi. Pamoja nae ameambatana na viongozi mbalimbali ikiwemo baadhi ya Mawaziri wakikaribishwa na mwenyeji wao Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama, na Mkuu wa Mkoa Wa Ruvuma Kanal Ahmed Abbas Ahmed
Idadi kubwa ya wananchi kutoka kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Songea, wameitikia wito, kwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Kanisa la Mtakatifu Joseph Peramiho.
Lengo kubwa ilikua ni kumshuhudia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa