Madiwani simamieni ukusanyaji wamapato katika Kata zenu
Madiwani watakiwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na miradi ya maendeleo inoyotekelezwa katika kata zao
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Songea Mhe Nelly Duwe amesema hayo katika kikao cha pamoja baina ya viongozi wa chama na wataalam mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea kilicho fanyika hivi karibu katika ukumbi wa Halmashauri hiyo .
Mhe Duwe amesema madiwani wasimamie ukusanyaji wa mapato na miradi ya maendeleo katika kata zao na kuendelea kudumisha ushirikiano baina yao na wataalam kwania ya kuhakikisha mapato ya Halmashauri yanaongezeka kutoka asilimia 51 na kuendelea pia usimamizi mzuri utasaidi sana mapato kuongezeka
Mhe Duwe amesema kila mtumishi awe wachama au wa Serikali anapaswa awajibika kutekeleza majukumu yake,na Serikali ya awamu ya tano haita mwonea haibu mtumishi yeyote mzembe kazini atachukua hatua kali za kisheria dhidi yake
Amesifu jitihada za uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa kutekeza ujenzi wa miradi kwa weledi mkubwa na kurekebisha kasoro ndogondogo zilizopo katika ujenzi wa miradi hiyo.
JACQUELEN CLAVERY-TEHAMA
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa