Mganga Mkuu wa Wilaya ya Songea Dr. Geofrey Kihaule leo tarehe 26/12/2024 amewakaribisha Madaktari Bingwa wa Macho kutoka Hospital ya Taifa Muhimbili Waliofika Songea DC kwa lengo la kutoa huduma kwa Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Akizungumza baada ya ujio wa Madakatari hao, Dr. Kihaule amesema “ Serikali imeendelea kuzingatia umuhimu wa Afya kwa wananchi wake kwa kuwarahisishia wananchi kukutana na Madaktari bingwa ili kuweza kuwatibu magonjwa mbalimbali.
Leo tunao Madakatari Bingwa wa Macho kutoka Hospital ya muhimbili ambao wamekuja kwa lengo la kusaisia wananchi wa Halmashauri wenye matatizo ya Macho”
Hata hivyo Dr. Kihaule ametoa wito kwa wananchi kutumia fulsa hiyo ya uwepo wa Madaktari hao ili kupata huduma kwan baada ya siku hizo nne, wataelekea Mikoa mingine hivyo kufanya mzunguko kuwa mkubwa.
Aidha ameshukuru Serikali ya Awam ya Sita, kwa mikakati mbali mbali ambayo wamekua wakiitumia katika kufikia na kusaidia wananchi
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa