• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE YAANZA SONGEA DC

Tarehe ya Kuwekwa: February 29th, 2024

Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Kupitia Divisheni ya Maendeleo ya Jamii wameanza mchakato wa Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi.

Siku ya wanawake duniani, (8 Mach) hutumika kuwaunganisha wanawake wote duniani kujadili maswala mbalimbali kuhusu maswala yanayowahusu lakini pia kukutana pamoja kwa lengo la kusaidia jamii kwa mambo yanayowazunguka ikiwa ni pamoja na matendo ya Huruma.

Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Kupitia Divisheni ya Maendeleo ya Jamii kama ilivyo kwa Halmashauri nyingine wamejipanga kuadhimisha siku hiyo kwa kufata maelekezo kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum ambapo pamoja na mambo mengine wamegawanyisha majukumu kwa kila siku kabla ya kufika tarehe 8 Marchi 2024.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Bi. Sophia Ndibahezwa amesema “ maandalizi ya siku ya wanawake duniani ambayo yataanza tarehe 1.03.2024 mpaka 8.03.2024, ambapo tarehe 1 machi tutakua na amsha hari ambapo kamati ya maandalizi itashirikiana na wananchi wa kata ya Liganga kufanya usafi kwenye ujenzi wa chuo cha walemavu kilichopo kwenye kata hiyo.

02.03.2024 Tutaenda kufanya matendo ya huruma kama inavyoelekeza Wizara, matendo hayo yatahusisha kutoa mahitaji kwa watu wenye mahitaji maalumu, lakini pia tutaenda kutoa chakula mavazi kwa watu walioathiliwa na ukoma. Sambaba na hili tarehe 04.03.2024 kutakua na kongamano la wanawake, ambapo wanawake kutoka sehemu tofauti watapata elimu ya Ujasiliamali, elimu ya fedha,  elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia, sheria za mirathi na umiliki wa mali, kizazi chenye usawa lakini pia elimu ya makuzi na malezi ya watoto kwa ajili ya ustawi wa familia zetu.

Aidha tarehe 06.03.2024 tutafanya uzinduzi wa siku ya wanawake katika Halmashauri ya Wilaya ya songea tutayafanya katika kata ya Liganga ambapo wananchi wote watashiriki. Maadhimisho haya kwa mwaka 2024 yanaongozwa na kauli mbiu “ Wekeza kwa Wanawake kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii”. Kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha Jamii kuwekeza kwa Wanawake ili kuleta Usawa wa Kijinsia pamoja na kukumbushana umuhimu wa usawa wa kijinsia katika kuchochea ukuaji wa Uchumi, Maendeleo Jumuishi na Ustawi wa Jamii kwa Maendeleo endelevu kwa Wanawake.

Hivyo siku ya kilele ambapo ni tarehe 08.03.2024, wanawake wote kutoka Wilaya zote Mkoa wa Ruvuma tutakutana Wilaya ya Mbinga kwa ajili ya Kuadhimisha siku hiyo.

Divisheni ya Maendeleo ya jamii imepongeza na kushukuru mchango uliotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mwl. Neema Maghembe kwa kufanikisha shughuli hiyo.

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAAFISA HABARI KIMEMALIZIKA KWA KUWEKA MAKUBALIANO ENDELEVU KWA MASLAHI MAPANA YA NCHI

    May 24, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA, WANATEGEMEA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA NA UBINGWA BOBEZI KATIKA HOSPITALI YA HALMASHAURI SONGEA

    May 21, 2025
  • MKIMBIZA MBIO ZA MWENGE KITAIFA, AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    May 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SONGEA DC, LIMEMSHUKURU MHE. RAIS NA WAZIRI WA AFYA KWA KUIHESHIMISHA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    April 29, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa