Maafisa watendaji wa kata na vijiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma wamepatiwa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo mpya wa ukusaji wa mapato.
Mafunzo hayo yametolewa na Afisa Tehama wa Halmashauri Bw John Luoga,yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea uliopo katika Mji mdogo wa Peramiho
Luoga amesema lengo kuu la kutoa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watendaji ili waweze kusimamia vizuri mfumo mpya wa ukusanyaji mapato na kudhibiti upotefu wa mapato ya serikali.
Amesema mfmo mpya wa ukusanyaji mapato umerahisisha matumizi na uandaji wa taarifa na hauruhusu mtumiaji wa mfumo kufanya kazi nje ya mfumo wa kukusanyia mapato.
Ametoa wito kwa watumiaji wa mfumo huo kuzingatia miongozo ya serikali ya ukusanyaji wa mapato kwa weledi mkubwa , sheria na taratibu za fedha.
Kwa upande wao wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kufanya kazi kwa weledi na kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao ya kazi na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani.
JACQUELEN CLAVERY
K /AFISA HABARI SONGEA -DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa