UFAULU WA SHUKA
Idara ya elimu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea Imetakiwa kuaondoa changamoto zinazosababisha ufaulu kushuka.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgeama katika kikao cha tathimini ya elimu kilicho fanyika hivi karibuni katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Maposeni.
Mgema amesema idara ya elimu ya Halmashauri ihakikishe inaondoa changamoto zinazopelekea kiwango cha taaluma kushuka kutoka nafasi ya tano kwa mwaka uliopita na kushika nafasi ya 7 mwaka 2018,kwakufanya ufuatiliaji na kutatua changamoto zinazo wakabili walimu pamoja na kuwapatia stahiki zao.
“sitataki kuona watoto wanashindwa kufaulu katika Wilaya yangu,nataka ufaulu kwa darasa la nne na lasaba uwe wa asilimia miamoja”,alisema mgema.
Mgema amesema walimu wanamatatizo mengi hivyo matatizo yote yanayowakabili walimu yapelekwa ofisini kwake kwa maandishi ili aweze kuyafanyia kazi
Shuleni 17 kati ya shule 69 za halmashauri zimeshindwa kufikisha wastani wa ufaulu waasilimia 50 nakusababisha halmashauri kushika nafasi ya 7 kimkoa,kufuatia kadhi hiiyo amemtaka mkrugenzi mtendaji kuzifuatilia shule hizo na kubaini matatizo katika shule hizo.
Wakitoa utetezi wa kushindwa kufikia malengo ya kufaulisha baadhi ya walimu wakuu wamesema wanakumbana na changamoto nyingi ikiwemo ya wazazi kuwakataza watoto wao wasijibu maswali kwa usahihi kwakuwa wao hawana uwezo wa kumudu gharama za mahitaji ya shuleni wanapo faulu.
Kitendo cha kuwashawishi watoto wasijibu maswali kwa usahihi ni miongoni mwamatendo ya kikatili kwa watoto kwakuwa yanakatisha ndoto za maisha za watoto na kuwasababishia umaskini, kitendo ambacho hakikubaliki katika jamii.
Jacquelen Clavery. 12/02/2019
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa