KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Abdalla Shaib Kaim amezindua mradi wa chemchem ya asili iliyoboreshwa iliyopo katika Kijiji cha Mpitimbi B ambacho kimetekelezwa na wanufaika wa mradi wa TASAF.
Aidha, Chemchem hiyo inauwezo wa kutoa lita 13,845 za maji kwa saa ambayo inanufaisha kaya 59 wanaoishi katika Vitongoji vya Baraza B na Mchekeni pia RUWASA wamechangia kuboresha chemchem hivyo gharama za mradi ni shilingi milioni 2,211,000.
Akizungumza katika uzinduzi huo amesisitiza wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la upandaji wa miti katika maeneo hasa yaliyo karibu na vyanzo vya maji kama hatua muhimu zinazotokana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo inaharibu na kuathiri mazingira na katika kutekeleza agizo la Serikali la utunzaji mazingira.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa