Kikao cha lishe Bora kwa kipindi cha Robo ya Tatu kwa mwaka wa Fedha 2023/2024, kilichokaa tarehe 8/05/2024 katika ukumbi wa Halmashauri Kimeazimia mikutano yote itakayofanyia kwenye Halmashauri hiyo kutolewa elimu ya Lishe Bora kwa wananchi.
Kikao hicho ambacho huratibiwa na Divisheni ya Afya, kwa kuambatata na wataalam wengine, ikiwemo watendaji wa kata zote 16 za Halmashauri ya Wilaya ya Songea kiliongozwa na Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndg. Mtela Mwampamba.
Elimu ya lishe bora na ulaji unaofaa indeekuolewa kwa jamii kupitia Mikutano yote ya Hadhara, Makongamano, Semina na Mashuleni pamoja na umuhimu wa kufanya mazoezi kwa jamii yetu yote. Mtela Mwampamba Katibu Tawala Wilaya ya Songea
Akifunga kikao hicho Ndg. Mwampamba alisema “tumekubaliana kwamba sasa na itabidi elimu ya Lishe bora itolewe kwa wananchi, hivyo naomba muandike barua kwa watendaji wote na wataalamu kuwa na kipengele cha Lishe bora kwenye kila mikutano yao ya ndani na nje.
Tumuombe pia Mbunge wa Jimbo la Peramiho na Kamatoi ya Siasa ya Wilaya kuweka kipembele cha Lishe kwenye mikutano yao ili kuhakikisha wananchi wanapata elimu juu ya Lishe bora”
Aidha walisistiza pia walimu wakuu wa Sekondari na Msingi, kuhakikisha wanalima bustani za mboga mboga kwenye maeneo yao ya shule ili kuwa na uhakika wa mboga za majaji kwa wanafunzi.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa