Mratibu wa magonjwa ya kifua kikuu na Ukoma wa Halmashauri ya Wiliya ya Songea mkoani Ruvuma Adam Ngunga amesema ugonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma bado ni tatizo kubwa katika Halmashauri hiyo.
Ngunga amesema takwimu za maambukizi ya magonjwa hayo zimekuwa zikiongezeka kila mwaka kwa wastani wa wagonjwa 210 hadi 230.
Ngunga amesema ugonjwa wa Ukoma na Kifua kikua ni magomjwa ambayo huambukizwa kwa njia ya hewa na yanaathari nyingi kwa mgonjwa ikiwemo ya kupata ulemavu kwa mtu anayeugua Ukoma.
Ngunga ameyataja maeneo ambayo yameathirika zaidi na tatizo la ugonjwa wa Ukoma kuwa ni kata ya Muhukuru kutokana na mwingiliano wa wagonjwa wanaotoka Nchi ya Msumbiji kuja kufuata huduma za matibabu ya ugojwa huo Tanzania.
Maeneo mengine kuwa ni Magima, Litisha na Morogoro kutokana na maeneo hayo kuwa ni kambi ya wagonjwa wa Kifua kikuu na Ukoma, hivyo kusababisha watu wengi kuambukizwa vimelea vya magonjwa hayo kwakuwa karibu na waathirika .
Amesema mtu yoyote anaweza ambukizwa vimelea vya magonjwa hayo kulingana na kinga ya mwili wake na wale wenye kinga pungufu ya mwili wapo hatarini zaidi ya kuambukizwa vimelea vya magonjwa hayo na kuugua ukilinganisha na wenye kinga imara.
Ngunga amezitaja dalili za ugonjwa wa ukoma kuwa ni mabaka mabaka yenye michoro tofauti tofauti kwenye mwili na endapo ukiwa na dalili hiyo nenda katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa hatua za kimatibabu na kikohozi cha muda mrefu kinachoambatana na homa hiyo ni kwa upande wa kifua kikuu.
Ameitaja mikakati ya kukabiliana na matatizo hayo ni pamoja na wagojwa wanaofika katika Vituo vya kutolea huduma za Afya kwa ajili ya matibabu kupimwa vimelea vya magonjwa hayo , kuendelea kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya vimelea vya ukoma na kifua kikuu pamoja na kuhamasisha jamii kujenga utamaduni wa kupima na kutibu dalili za magojwa.
Tiba na uchunguzi wa magonjwa hayo hutolewa bure katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari
Songea dc.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa