Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya jamii Tanzania (Tanzania Social Action Fund) TASAF, imetoa zaidi ya Bilion 1.3 kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu mbalimbali katika Halmasahuri ya Wilaya ya Songea
Halmashauri ya Wilaya ya Songea ni moja kati ya Halmashauri 8, katika Mkoa wa Ruvuma zinazotekeleza mpango wa kunusuru kaya maskini. Hata hivyo Halmashauri hiyo imepokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu.
Akizungumza kwa niaba ya Halmashauri, Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bi. Hossana Ngunge anasema
“ Zaidi ya Bilion moja zimeletwa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo”
Akiitaja Miradi hiyo, Bi. Hossana amesema
“Halmashauri imepokea kiasi cha Tsh. 185,713,178.57 kwa ajili ya ujenzi wa soko katika kijiji cha Peramiho A, kata ya Peramiho. Soko hilo lina vizimba 82, na kwa sasa linatumika.
Imepokea pia kiasi ya Tsh 68,675,00 kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba ya Mganga katika hospital ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Zahanati ya Mdundualo iliyopo kijiji cha Mdundualo kata ya Maposeni, imepokea kias cha Tsh. 170,995,797.32 kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba 2 za watumishi wa Afya, Matundu 6 ya vyoo na kisima kirefu cha maji.
Kijiji cha Parangu kilichopo kata ya Parangu, kimepokea kiasi cha Tsh. 339,161,371.43 kwa ajili ya ujenzi wa Stendi ya Mabasi.
Hata hivyo kiasi cha Tsh. 686,367,802.68 Kimeletwa ili kujenga Stendi ya kisasa katika kijiji cha Lundusi kata ya Peramiho na ujenzi huo upo hatua ya mwisho.
Aidha Mratibu amemshkuru sana Mhe. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia kaya Maskini lakini pia Halmashauri ya Wilaya ya Songea,
Amemshkuru pia Mbunge wa Jimbo la Peramiho na Madiwani kwa kuendelea kuhakikisha wananchi wanafanikiwa kupitia TASAF.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa