Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Ndg. Mtela Mwampamba, amewataka Wananchi wa wilaya ya Songea kukata Bima ya Afya kwa ajili ya kuwa na uhakika wa matibabu na Afya zao.
Mwampamba ameyasema hayo jana 17.07.2024 alipopata nafasi ya kuzungumza kwenye Mkutano wa hadhala wa Mbunge wa Jimbo la Peramihoi uliofanyika katika kijiji cha Nakahuka na Morogoro katika kata ya Litisha.
“ Ndugu zangu wananchi, najua sasa wengi mmevuna mahindi, maharage nk, naamini kwa sasa mnauwezo wa kukata bima hata zile za elfu thelathini ( 30,000/=) ambazo zinaweza kutibu watu sita. Hivyo nitoe wito kwa wananchi wote mjitahidi kuwa na bima ya afya ili kujiwekea uhakika wa kuopata matibabu wakati wote .
Aidha katibu tawala alisisitiza tena kuhusu upatikanaji wa yeti vya kuzaliwa, hii ni baada ya wananchi wengi kujazana ofisi ya Mkuu wa Wilaya kutafuta vyeti pindi wanapopata changamoto au wanahitaji kujiunga ya shile au ajila.
Niwakumbushe pia sasa unaweza kupata cheti cha kuzaliwa kupitia simu yako Simu janja ( Smart Phone) hivyo kwa sasa punguzeni safari zakwenda mpaka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwani kule mnakua mnatumia fedha na muda wenu, cha msingi tembeleeni ofisi ya mtendaji ili awape maelekezo namna ya kupata chet cha kuzaliwa kuputia simu zenu.
Katibu tawala amekua akiambatana na Mbunge wa Jimbo lka Peramiho kwenye Ziara yake ya kuzungumza na wananchi waliopo Halmashauri nya Wilay ya Songea
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa