Kamati zinazosimamia ujenzi wa hospitali ya wilaya ya songea zimetakiwa
Kujiepusha na hujuma mbalimbli ambazo zitakwamisha mradi wa ujenzi kutokamilika kwa wakati.
Kauli hiyo imetolwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya songea mkoani Ruvuma Bw Simoni Bulenganija katika kikao elekezi cha kuzitambua kamati na jinsi namna zitakavyo tekeleza majukumu yake,kilicho fanyika hivi karibuni kwenye ukumbu wa Halmashauri hiyo.
Bw Bulenganija amewataka wanakamati kjiepusha na vitendo vya hujuma ambavyo vitakwamisha mradi kutokakamilika kwa wakati au utekelezaji wake kuwa chini ya viwango,watakapo ona viashiria vya hujuma yoyote watoe taarifa kwa uongozi wa Halmashauri kwa ajili ya ufutiliaji na kuchukua staiki.
Amesema kazi ya ujenzi wa mradi huo unahitaji uadilifu na uzalendo ni vizuri kamati zote zikafanya kazi kwakushirikiana na kuacha misuguano isiyokuwa na tija ambayo itachelewesha kazi kufanyika.
“sipendi kuona watu mkichongeana na kuhujumiana jambo la msingi ni kuweka nia njema ya kufanya kazi”,alisema Bulenganija.
Afisa mipango wa Halmashauri ya wilaya ya songea Bw Richard Masesa alieleza na kufafanua miongozo iliyotolewa na OR-TAMISEMI inayoelekeza uundaji wa kamati na majukumu ya kila kamati itakavyo tekeleza majukumu yake,jumla ya kamati tano zimeundwa kwa ajili ya usimamizi na ufutiliaji wa maradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya songea ambayo itajengwa Kijiji cha Mpitimbi B Kata ya Mpitimbi Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea ni miongoni mwa Halmashauri 67 nchini zilizo pata fedha toka OR -TAMISEMI kwa ajili ya ujenzi wa haspitali za wilaya, Halmashauri ya Songea imepata sh.bilioni moja na milioni miatano.
Jacquelen Clavery –Habari –Tehama.12/02/2019.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa