• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya

KAMATI zatakiwa kuwa makini katika kusimamia miradi

Tarehe ya Kuwekwa: March 16th, 2023

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mheshimiwa Menas Komba amezitaka kamati zinazosimamia miradi katika ngazi ya Kata na Kijiji kushiriki kikamilifu kusimamia miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao.

Ameyasema hayo katika kikao cha kutoa mafunzo kwa kamati za ujenzi kwa Kata ambazo zimepokea fedha za kutekeleza miradi kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Lundusi-Peramiho.

Pia lengo la kikao ni kuzitambua kamati ambapo wataalamu kutoka Idara ya ujenzi na manunuzi wametoa mafunzo namna ambavyo kamati zinatakiwa kutekeleza majukumu yake.

Akizungumza Mheshimiwa Komba amewataka wanakamati kujiepusha na vitendo vya hujuma ambavyo vitakwamisha miradi kutokukamilika kwa wakati au utekelezaji wake kuwa chini ya viwango.

Ameongeza kuwa katika ujenzi wa miradi hiyo uzalendo ni kitu cha muhimu hivyo amezitaka kamati za ujenzi kwa kushirikiana na Viongozi wa Kata na Vijiji pale ambapo nguvu za wananchi zinahitajika basi waweze kuwashirikisha na kuwasisitiza ili washiriki kikamilifu.

``Kamati ambazo mnaenda kusimamia ujenzi mkawe makini sana katika kuwasimamia mafundi viongozi hakikisheni kila fundi anaandaa mpango kazi kwani itasaidia sana kujua utendaji kazi wao pia miradi itakwenda kukamilika kwa wakati’’, amesisitiza Mheshimiwa Komba.

Kwaupande wake Kaimu Mkurugenzi Bi Bumi Kasege amewataka mafundi viongozi kushiriki ujenzi kuanzia mwanzo hadi mradi utakapokamilika na sio kuwaachia mafundi wasaidizi ambao wanaweza wasiwe wataalamu na mradi usikamilike kwa viwango vinavyotakiwa.

Vilevile amezisisitiza kamati kununua na kutumia vifaa vyenye viwango vinavyokubaliwa na Serikali na kama ambavyo vimeelekezwa kwenye muongozo wa BOQ.

Nae mtaalamu kutoka ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Bw Patrick Mtavangu amezitaka kamati kutokutengeneza nyaraka za uongo kwa lengo la kumdanganya mwajiri kwani ni kosa hivyo amewahasa kuwa waaminifu katika kusimamia miradi hiyo na wasiwe chanzo cha kukwamisha miradi.

Pia amesisitiza mafundi wasilipwe fedha kabla ya mradi kukaguliwa na wasilipwe fedha za ziada hivyo walipwe fedha zilizoandikwa kwenye mkataba.

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO October 12, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • TAARIFA ya mapokezi ya fedha kiasi cha Shilingi Milioni 55 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa Songea DC.

    March 23, 2023
  • KAMATI zatakiwa kuwa makini katika kusimamia miradi

    March 16, 2023
  • TANGAZO LA KAZI

    March 09, 2023
  • ZIARA ya Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Ndile Songea DC

    March 07, 2023
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa