KAMATI ya siasa ya Mkoa wa Ruvuma ya kagua miradi ya maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Kamati ya siasa ya Mkoa wa Ruvuma yaagiza miradi inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea ikamilishwe na ianze kutoa huduma kwa Wananchi kwa hatua za awali kabla ya Agosti mosi 2020
Maagizo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ndugu Oddo Mwisho wakati wa ukukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekekelezwa katika halmashauri hiyo iliyofanyika Julai sita ,2020.
Mwisho amesema azima ya Serikali kuona wananchi wanapata huduma kama vile huduma za afya,maji safi na salama ,mazingira mazuri ya kutolea elimu ,barabara na huduma nyingine za kijamii ambazo wanamchi wanastahili kupata.
“Napongeza hatua za utekelezaji wa miradi unavyoendelea majengo mazuri yaende sambamba na utoaji wa huduma inayotakiwa kutolewa”alisema Mwisho.
Naye katibu wa CCM wa Mkoa wa Ruvuma Nuru Ngereja ametoa wito kwa wataalam wa Halmashauri hiyo kutnza miundombinu ya miradi hiyo ili iweze kudumu na kutoa huduma endelevu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw Simon Bulenganija amehaidi kusimamia kufuatilia na kushugulikia miradi yote ya Afya iliyotembelewa na kuhakikisha inaanza kutoa huduma iliyo kusudiwa kwa wakati.
Miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni ujenzi kituo cha Afya Magagura,,Hospitali ya Wilaya Mpitimbi,ujenzi wa vyoo vilivyo boreshwa kupitia mradi wa SHWASH katika Kijiji cha Mpitimbi,miradi mingine ni ujenzi wakituo cha Afya Muhukuru ambacho kimeanza kutoa huduma za upasuaji kuanzia Aprili mosi 2020,mradi wa maji katika Kata ya Muhukuru Lilahi na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi kilichopo Muhukuru Lilahi.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa habari Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa