KAMATI ya fedha, uongozi na mipango ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Menas Komba imefanya ziara katika Wilaya ya Songea kata ya Ndongosi kijiji cha Nambendo.
Aidha katika ziara hiyo wametembelea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na Serikali ya awamu ya sita na kusimamiwa na uongozi wa Halmashauri.
Waheshimiwa Madiwani wametembelea shule ya msingi Nambendo ambapo ujenzi ulifanyika kupitia mradi wa EP4R shule ilipokea shilingi Milioni 87,700,000 kwaajili ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, ofisi mbili za walimu, vyoo matundu saba pamoja na kutengeneza madawati 60.
Akizungumza Mhe.Menas ameutaka uongozi wa shule ufanye ukarabati wasakafu kwa madarasa mawili na kumalizia kuweka vioo katika sehemu ya juu ya milango kwa haraka.
Ametoa rai kwa walimu kufanya jitahada za kuhakikisha wanafunzi wanaudhuria shuleni na kushiriki kikamilifu katika masomo ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.
“Kuna kila sababu ya kufanya juhudi, mikutano ya wazazi ili kuhakikisha wanafunzi wote wanakuja shuleni na kuhudhuria vipindi darasani maana faida ya Serikali ni kuona watoto wakisoma na wanafaulu vizuri ndio maana inaboresha miundombinu”,amesema Mhe.Menas.
Waheshimiwa Madiwani wametembelea na kukagua ujenzi wa nyumba ya mwalimu ambayo imejengwa na nguvu za wananchi wakishirikiana na uongozi wa Halmashauri na Mfuko wa Jimbo .
Pia Waheshimiwa Madiwani wametembelea Zahanati ya Nambendo ambayo Serikali ilileta fedha kiasi Cha shilingi Milioni 24 kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa matundu Saba ya vyoo, bafu moja, jengo la mama na mtoto pamoja na kujenga mnara wa kukalishia tenki la maji.
Vilevile Waheshimiwa Madiwani wametembelea na kukagua eneo la shamba lenye ukubwa wa hekari 1000 na kuangalia mipaka ya shamba hilo.
Uongozi wa shule ya msingi Nambendo umetoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kwa kusaidia kuleta fedha kwaajili ya kutekeleza miradi hiyo.
Pia wamewashukuru baraza la Madiwani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Menas Komba, Timu ya wataalamu wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Neema Maghembe, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi na uongozi wote wa kata na Kijiji kwa kusaidia kutekeleza miradi hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa