Idara ya maendeleo ya jamii ikiongozwa na Bi Zawadi Nyoni wametoa mafunzo na kujenga uelewa juu ya ujasiliamali kwa vikundi ambavyo vinapokea mikopo ya asilimia 10 katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Mafunzo hayo yametolewa katika ukumbi wa Halmashauri Lundusi-Peramiho.
Bi Zawadi amesema mikopo ambayo imetolewa kwa mwaka 2022/2023 ni kiasi cha shilingi Milioni 159,233,630.22.
Ameongeza kuwa idadi ya vikundi ambavyo vimepokea fedha ni 25, ikiwa vikundi vya vijana vipo 10, wanawake vipo 10 na watu wenye ulemavu vipo 5.
“ Tumefanya ufuatiliaji kwa vikundi tulivyowapa mikopo na kubaini kuwa wanajishughulisha na shughuli mbalimbali zikiwemo kilimo na ufugaji, ujasiliamali, shughuli za usafirishaji pamoja na Viwanda vidogo vidogo”, amesema Bi Zawadi.
Akizungumza katika mafunzo hayo amesisitiza vikundi hivyo kurudisha fedha kwa wakati ili ziweze kukopeshwa kwa vikundi vingine vyenye uhitaji.
Wakizungumza wanufaika wa mikopo hiyo wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama na uongozi wa Halmashauri kwa kuendelea kutoa mikopo ambayo inawasaidia kuendesha shughuli mbalimbali ambazo zinawawezesha kujikimu kimaisha.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa