• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

HOSPITALI ya Wilaya ya Songea inatarajia kuanza kutoa huduma ifikapo Julai 15 /2020

Tarehe ya Kuwekwa: July 8th, 2020

 HOSPITALI ya Halmashauri ya Wilaya Songea mkoani Ruvuma ambayo imejengwa katika kijiji cha Mpitimbi B kwa gharama ya shilingi bilioni 1.8 inatarajia kuanza kutoa huduma za matibabu kuanzia Julai 15 mwaka huu.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo kwa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma katika eneo la mradi,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Simon Bulunganija amesema mradi huo umefikia asilimia 95 ya utekelezaji ambapo amezitaja huduma ambazo zitaanza kutolewa na hospitali hiyo ni za wagonjwa wa nje (OPD).

Amesema ujenzi wa hospitali hiyo ulianza mwaka 2019 na kwamba katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huo Halmashauri ilipokea shilingi bilioni 1.5 ambazo zilijenga hadi katika hatua ya ukamilishaji.

“Nachukua fursa hii kwa niaba ya wananchi wa Halmashauri ya Songea kumshukuru Rais Dkt.John Magufuli kwa kutuongeza shilingi milioni 300 na kufanya mradi kutumia sh.bilioni 1.8 kutekeleza mradi huu’’,alisema Bulenganija.

Hata hivyo amesema hadi sasa zimetumika zaidi ya shilingi bilioni 1.5 na kwamba wanatarajia majengo yote saba ya hospitali hiyo kukamilika Julai 30 mwaka huu na kuwezesha huduma zote za afya kuanza kutolewa katika hospitali hiyo.

Amesema hospitali hiyo inatarajia kuhudumia kata zote za Halmashauri ya Wila ya Songea ,hata hivyo amezitaja changamoto zilizopo katika mradi huo ni mgawo wa maji ambao husababisha mafundi kukwama kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo kwa wakati.

Ameyataja majengo ya hospitali hiyo yanayoendelea kukamlishwa kuwa ni jengo la utawala ambalo limefikia asilimia 90,jengo la wagonjwa wa nje asilimia 80,stoo ya dawa asilimia 92,ujenzi wa maabara asilimia 92,jengo la vipimo vya mionzi asilimia 85,jengo la kufulia asilimia 90 na jengo la wazazi asilimia 90.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa hospitali hiyo,Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho ameupongeza uongozi wa Halmashauri hiyo kwa kutekeleza mradi huo,hata hivyo amewaomba kuongeza kasi ili wananchi waanze kupata huduma hiyo.

“Sisi tunakimbizana na muda mwaka 2015 tuliwaahidi wananchi kwamba tutawasogezea huduma ya afya jirani hivyo tunataka wananchi waanze kupata huduma zote ili wakati wa Kampeni tuwaambie wananchi tuliahidi tumetekeleza’’,alisisitiza Mwisho.

Katika kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maji,Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA katika Wilaya ya Songea Mhandisi Samwel Sanya amesema wanatarajia kupeleka huduma ya maji katika hospitali hiyo ifikapo Julai 30 mwaka huu.

Naye Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu Sera,Mbunge,Ajira ,Vijana na Wenyeulemavu ambaye pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama ameutaja mpango wa muda mrefu wa kukabiliana na upungufu wa maji katika eneo la hospitali na wakazi wa kijiji cha Mpitimbi ni kuchimba visima virefu na kwamba fedha za kutekeleza mradi huo katika jimbo zima la Peramiho zimekwisha pokelewa.

      Imeandikwa na

JACQUELEN CLAVERY.

AFISA HABARI SONGEA DC.

         8/7/2020.

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAAFISA HABARI KIMEMALIZIKA KWA KUWEKA MAKUBALIANO ENDELEVU KWA MASLAHI MAPANA YA NCHI

    May 24, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA, WANATEGEMEA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA NA UBINGWA BOBEZI KATIKA HOSPITALI YA HALMASHAURI SONGEA

    May 21, 2025
  • MKIMBIZA MBIO ZA MWENGE KITAIFA, AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    May 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SONGEA DC, LIMEMSHUKURU MHE. RAIS NA WAZIRI WA AFYA KWA KUIHESHIMISHA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    April 29, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa