• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA YATINGA KWA KISHINDO UMISETA TAIFA

Tarehe ya Kuwekwa: June 18th, 2025


Huku Taifa likijiandaa na mashindano ya Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) yatakayoanza rasmi kesho tarehe 19 Juni 2025 mkoani Iringa, Halmashauri ya Wilaya ya Songea imeendelea kung’ara kama chachu ya maendeleo ya michezo kwa wanafunzi baada ya kutoa idadi kubwa ya wachezaji watakaoiwakilisha timu ya Mkoa wa Ruvuma.

Akizungumzia maandalizi ya mashindano hayo, Afisa Michezo wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Ndugu Francis Shuka, amesema “maandalizi yamekamilika na timu ya wanamichezo ipo njiani kuelekea Iringa huku viongozi wa msafara wakiwa tayari wamewasili kwa ajili ya maandalizi ya mwisho.

"Timu yetu imejiandaa kikamilifu na tunajivunia kutoa mchango mkubwa katika timu ya Mkoa, hususan katika mchezo wa pete ambapo tumetoa wachezaji 5 sawa na nusu ya timu nzima. Hii ni dhihirisho la juhudi zetu katika kukuza michezo mashuleni," amesema Shuka.

Mbali na mchezo wa pete, Halmashauri ya Wilaya ya Songea pia imetoa wachezaji 4 wa mpira wa miguu wa kiume, wachezaji 4 wa mpira wa miguu wa kike, pamoja na wachezaji 2 wa mpira wa kikapu kwa upande wa wanawake  hali inayodhihirisha kuwa vipaji vinaibuliwa kwa jinsia zote na katika michezo tofauti tofauti.

Katika hatua nyingine ya kuonyesha mshikamano na ushirikiano, Ndg. Shuka amewashukuru wazazi na walezi kwa kuwa mabalozi wazuri wa maendeleo ya michezo kwa watoto wao. Ameeleza kuwa uelewa wao juu ya umuhimu wa michezo katika makuzi ya wanafunzi umechangia mafanikio haya.

Aidha, ametoa wito mahsusi kwa wakuu wa shule kuendelea kutenga nafasi kwa wanafunzi wenye vipaji vya michezo, akisisitiza kuwa michezo si kikwazo cha taaluma, bali ni nyenzo muhimu ya kuinua ari ya kujifunza na nidhamu kwa vijana.

Katika hotuba yake, Shuka alimshukuru kwa dhati Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Bi Elizabeth Gumbo, kwa kuwa mstari wa mbele katika kusapoti jitihada za michezo. Vilevile alitoa shukrani kwa Idara ya Elimu, ikijumuisha elimu msingi na sekondari, kwa kushirikiana bega kwa bega katika kufanikisha safari hii.

Kwa mafanikio haya, Halmashauri ya Wilaya ya Songea imeendelea kuthibitisha kuwa ni kitovu cha vipaji na mfano wa kuigwa kitaifa, si tu katika taaluma bali pia katika kuinua michezo mashuleni. Mashindano hayo yamebeba kauli mbiu isemayo Viongozi Bora ni msingi wa Maendeleo ya Taaluma, Sanaa na Michezo, Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • VIKUNDI 28 VAPATIWA MIKOPO YA TSH MILIONI 249 NA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    July 03, 2025
  • ZAIDI YA MILIONI 600 ZIMETUMIKA KUJENGA STEND YA KISASA PERAMIHO

    July 01, 2025
  • Ujenzi wa Mradi wa Barabara Likuyufusi–Mkenda ni fursa mpya ya Maendeleo ya Songea Dc.

    June 20, 2025
  • WASIMAMIZI WA MIRADI WASISITIZWA KUZINGATIA UADILIFU NA UFANISI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MAENDELEO SONGEA DC

    June 19, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa