Zoezi la usajili, utambuzi na ufuatiliaji wa mifugo, lilizinduliwa na Mkuu wa wilaya ya Songea Ndugu. Pololet Mgema na amewataka wafugaji kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa na Serikali ili kujiepusha na migogoro.
Akiongea na wafugaji wa Mhepai, Mkurugenzi Mtenadaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea ndugu Simon Bulenganija amesema Halmashauri ya Wilaya imeanza kutekeleza agizo hilo la Serikali la kuzitaka Halmashauri kutambua na kusajili mifugo yote nchini chini ya sheria ya Bunge Na. 12 ya mwaka 2010 kwa mujibu wa kifungu cha 12(1) cha sheria ya utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo
Aidha Mkurugenzi amesema, malengo makuu ni kusajili na kutambua mifugo yote katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea pamoja na kuwa na takwimu sahihi za mifugo katika Halmashauri.
Usajili wa Mifugo utarahisisha upatikanaji wa takwimu za mifugo zitakazowezesha Halmashauri ya Wilaya ya Songea kupanga matumizi bora ya ardhi na uendelezaji wa nyanda za malisho pamoja na kupanga mahitaji ya madawa, chanjo na ujenzi wa miundo mbinu kama majosho, vibanio, malambo, minada na Ujenzi wa vituo vya huduma za afya ya mifugo.
Upatikanaji wa Takwimu sahihi za mifugo utasaidia kushawishi wawekezaji hasa wasindikaji na wadau wengine wa mazao ya mifugo kuwekeza katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea imejipanga kuimarisha mitandao ya mawasiliano katika kudhibiti wizi, upotevu wa mifugo, kuthibiti magonjwa na kuwezesha ufuatiliaji wa mifugo wakati wa ukomo wa umiliki na uhai wa mifugo kwenye minada na machinjio.
Takwimu hizi zitaingizwa katika kitabu, na baadae katika mfumo wa kompyuta ili kuwezesha utunzaji takwimu sahihi za mifugo. Inapotokea kukoma kwa umiliki kutokana na kuuza mifugo, uchinjaji, upotevu na wizi, taarifa hizi zitakuwa zinahuishwa mara kwa mara ili ziwe sahihi kila wakati.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa