Halmashauri ya Wilaya ya Songea imetembelewa na Mbunge anayesemea wafanyakazi na kutetea maslahi ya watumishi Bungeni Dkt. Alice Kaijage Novemba 13, 2023.
Mheshimiwa Dkt. Kaijage katika ziara yake ameweza kusikiliza kero mbalimblai za watumishi na kwenda kuzisemea Bungeni, Aidha Mheshimiwa Dkt. Kaijage ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutatua baadhi ya kero za watumishi kwa kuwapandisha vyeo na madaraja mbalimbali.
Mheshimiwa Dkt. Kaijage amesema “katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali ilitenga bajeti kwa ajili ya kuwapindisha vyeo watumishi 12,000, na pia imeweza kuwabadilisha Kada (Muundo) watumishi mbalimbali na kiasi cha Shilingi Bilioni 2.5 zimetumika”.
Pia Mheshimiwa Dkt. Kaijage amefafanua juu ya suala la ajira na kwamba tangu Mheshimiwa Dkt. Rais Samia suluhu Hassan ameingia madarakani ameweza kutoa ajira katika nafasi mbalimbali zaidi 47,374 na bado ataendelea kutoa nafasi za ajira kwa Watanzani, Mwaka wa Fedha 2023/2024 Serikali imetenga nafasi za ajira 27,000 za nafasi mbalimbali.
Mheshimiwa Dkt. Kaijage amewaomba watumishi kuwa na imani ya kufanya kazi kwa uadilifu na kuiombea amani Nchi ya Tanzania.
Nae Afisa Utumishi wa Halmashauri Ndugu Hashim Lugome ambaye amemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji aliweza kutoa ufafanuzi wa mambo kadhaa ambayo yalitolewa kama hoja na baadhi ya watumishi.
Vilevile ametoa shukrani kwa Mhe. Kaijage kwa kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Songea na kusikiliza kero za Watumishi.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa