Naibu Katibu Mkuu Elimu Ofisi ya Raisi TAMISEMI Dkt. Charles Msonde amepongeza maendeleo ya ujenzi wa miundombinu katika shule ya sekondari Maposeni wakati akikagua miradi inayojengwa kwa ufadhiri wa kampuni ya BARRICK GOLD MINE TANZANIA.
Ukaguzi huo umefanyika leo tarehe 22/11/2023 ambapo naibu katibu mkuu amekagua madarasa 4 yenye thamani ya shilingi 96,000,000, mabweni mawili yenye thamani ya shilingi 256,000,000 na matundu 6 ya vyoo yenye thamani ya shilingi 10,200,000 na kufanya jumla ya majengo yote thamani yake ni shilingi 362,200,000. Ambapo amesema
“Kwa kweli niwapongeze kwa hatua mliyoifikia kwasababu ubora wa majengo unaonekana hii inaashiria mnae mhandisi makini, pia niwapongeze wote ambao mmeshirikiana mpaka kufika hapo ambapo majengo yalipofikia niwaombe tu ongezeni jitihada katika sehemu hii iliyobakia ili majengo haya yaanze kutumika”
“Kipekee tumshukuru Mbunge wa Jimbo la peramiho Mhe Jenista Mhagama kwa jitihada zake kwamaana yeye ndiye aliyefika kuomba fedha za ujenzi wa miundombinu hii na kwasababu serikali yetu ni sikivu basi haikusita kuelekeza fedha hizo katika kujenga miundombinu kwenye shule hii.” Alisema Cherles Msonde Naibu Katibu Mkuu-Elimu Ofisi ya Raisi TAMISEMI.
Nae Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndg Neema M Maghembe amemshukuru kwa ujio wa naibu katibu mkuu na kwa kutembelea miradi hiyo na kuahidi kukamilisha miradi hiyo kwa wakati ikiwa ni pamoja na ifikapo tarehe 15 disemba mwaka huu majengo hayo yatakuwa yamekamilika kwani vifaa vyote vipo gharani.
Akisoma taarifa ya utekeleaji wa ujenzi wa miundomdinu hiyo Mkuu wa shule ya sekondari maposeni Mr. Dismas Nchimbi amesema shule ilipokea jumla ya kiasi cha shilingi 362,200,000 kwaajili ya ujenzi wa madarasa manne, mabweni mawili na matundu sita ya vyoo, ambapo mpaka sasa majengo yote yapo katika hatua za ukamilishaji na kiasi cha fedha kilichobaki ni shilingi 103,886,000.
Pia amemshukuru Mhe. Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuruhusu fedha hizo zielekezwe katika shule hiyo, pia Mbunge wa jimbo la peramiho Mhe Jenista Mhagama kwa kuendelea kulipigania jimbo la peramiho, pia amelishukuru baraza la madiwani likiongozwa na Mwenyekiti wake wa Halmashauri Mhe Menasi Komba, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri na timu yake kwa ufuatiliaji wake mzuri.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa