Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Ndugu Petter Miti, amezindua mafunzo maalum ya utoaji wa mikopo ya asilimia kumi inayotokana na mapato ya ndani kwa Watumishi ngazi ya Kata Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Mafunzo haya yamefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Maposeni na yanalenga kuwajengea uwezo watumishi wa ngazi ya kata kusimamia utoaji wa mikopo hii.
Katika hotuba yake, Ndugu Miti aliwaeleza washiriki kwamba Serikali imewaamini watumishi wa ngazi za kata kusimamia zoezi hili, na hivyo amewataka wahakikishe wakopaji wanapata elimu ya kutosha kuhusu mikopo hiyo kabla ya kupewa. Alisisitiza umuhimu wa kuwapa wananchi elimu juu ya jinsi mikopo hiyo ilivyokuwa miaka ya nyuma na mabadiliko yaliyopo sasa katika utoaji wa mikopo hiyo.
Aidha, kaimu Mkurugenzi huyo alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa wakopaji wanarejesha mikopo kwa wakati. “Hakikisheni mkopaji anarudisha mkopo kwa wakati ili wengine pia waweze kupata nafasi ya kukopa,” alisema Ndugu Miti.
Mikopo hii inalenga kutoa fursa kwa wanawake, vijana, na walemavu katika jamii, ikiwa ni juhudi ya serikali kuwasaidia kufikia malengo yao ya kiuchumi na kujitegemea.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa