• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

POLOLETI MGEMA AAGIZA Halmashauri kutenga fedha kwaajili ya kutekeleza afua za lishe

Tarehe ya Kuwekwa: July 3rd, 2021

Mkuu wa Wilaya Songea Mkoani Ruvuma Pololeti Mgema ametoa agizo kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma kutenga fedha za mapoto ya ndani kwa ajili ya kutekeleza afua za lishe katika Halmashauri hiyo.

Mgema ametoa agizo katika kikao cha tathimini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe kilicho fanyika hivi karibuni   katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Mgema ametoa agizo hilo kufuatia viashiria vya lishe kutotekelezeka kwa ufanisi katika jamii ambapo Serikali ngazi ya Mkoa hadi Watendaji wa Vijiji walisaini mkataba mwaka 2019 wa utekeleza wa afua za lishe kwa lengo la kufanikisha mapambano dhidi ya lishe duni tatizo  ambalo bado lipo katika jamii.

“Ukweli ni kwamba lishe ni swala mtambuka na utapiamlo ni matokeo ya mkusanyiko wa matatizo mengi, “amesisitiza Mgema.

Mgema amefafanua kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kuwekeza kwenye lishe kama msingi imara na mkakati wa kufanikisha shughuli za kiuchumi ambazo zitatuwezesha kufikia uchumi wa kati wa viwanda endapo tu wananchi wake watakuwa na afya bora na wenye uwezo wa kufanya kazi.

Mgema ameyataja matokeo ya lishe duni ni utapiamlo ambao unasababishwa na ulaji duni,maradhi mbalimbali,kukosa uhakika wa kupata chakula katika jamii,matunzo duni kwa mama mjamzito tangu siku ya kutunga mimba hadi kujifungua ,mazingira duni ,machafuko ya kisiasa,mgawanyo wa rasilimali  usio zingatia uwiano wa kijinsia na mazingira machafu.

Mgema amezitaja baadhi ya afua za lishe ambazo zinatakiwa kutekelezwa na hazitekelezwi ipasavyo katika kupambana na tatizo la lishe duni kwenye jamii kuwa ni utapia mlo mkali,upimaji wa watoto sehemu ya juu ya mkono,utekelezaji wa vikao vya kisheria vya lishe,usimamizi shirikishi wa lishe,na utoaji wa matone ya vitamini A kwa watoto chini ya miaka mitano

Mgema ameyataja makundi ambayo yanaonekana kuathirika na tatizo la lishe duni kuwa ni Watoto chini ya miaka mitano ,wanawake walio katika umri wa kuzaa wa miaka 15-49,wanawake wajawazito ambao baadhi yao  wanakabiliwa na changamoto ya kujifungua watoto njiti na wenye mtindio wa ubongo na upungufu wa damu.

Ameongeza kwa kusema takwimu zinaonyesha kuwa Halmashauri inatatizo la udumavu wa asilimia 37.4, uzito pungufu upo kwa asilimia 13, ukondondefu asilimia 18.5, uzito mkubwa kwa wanawake na wanaume ni asilimia 21.1 na upungufu wa damu kwa akinamama wenye umri wa kuzaa ni asilimia 14, na Watoto chini ya miaka mitano ni asilimia 21.

Kwa upande wake Afisa lishe wa Halmashauri hiyo Joyce Kamanga amesema lishe sasa ni swala kimaendeleo Nchini mapambano dhidi ya lishe duni ni moja ya maeneo ya kipaumbele ya miaka mitano (2016/17-2020/21); mpango wa unaolenga kutekeleza Dira yetu ya maendeleo ya mwaka 2025.

Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma inawatoto elfu 21 ambao wanatakiwa kutengewa fedha kwaajili ya utekelezaji wa afua za lishe kwenye ngazi ya Kata ambako ni kitovu cha utekelezaji wa afua hizo.

Imeandaliwa na kuandikwa na

Jacquelen Clavery

Afisa Habari Songea dc.

  

 

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAAFISA HABARI KIMEMALIZIKA KWA KUWEKA MAKUBALIANO ENDELEVU KWA MASLAHI MAPANA YA NCHI

    May 24, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA, WANATEGEMEA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA NA UBINGWA BOBEZI KATIKA HOSPITALI YA HALMASHAURI SONGEA

    May 21, 2025
  • MKIMBIZA MBIO ZA MWENGE KITAIFA, AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    May 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SONGEA DC, LIMEMSHUKURU MHE. RAIS NA WAZIRI WA AFYA KWA KUIHESHIMISHA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    April 29, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa